Badilisha upendavyo utumiaji wako wa Showmax kwa kuunda wasifu kwa kila mmoja wa wanafamilia wako, wakiwemo watoto wako wadogo.
Wasifu unaweza kuundwa na kubadilishwa kwenye skrini ya Wasifu.
Unda wasifu
- Ingia kwenye showmax.com au uanzishe programu ya Showmax.
- Fikia skrini ya Wasifu kupitia aikoni ya Wasifu kwenye sehemu ya viungo muhimu.
- Sogeza au telezesha kidole kulia, kisha ubofye kwenye aikoni ya + ili kuunda akaunti mpya.
- Chagua ishara.
- Chagua Ndiyo au Hapana kwenye swali la Wasifu wa Watoto.
- Kisha andika jina la wasifu na ubofye Nimemaliza.
Dhibiti Wasifu
- Ingia kwenye showmax.com au uanzishe programu ya Showmax.
- Fikia skrini ya Wasifu kupitia aikoni ya Wasifu kwenye sehemu ya viungo muhimu.
- Chagua wasifu unaotaka kubadilisha.
- Bofya kwenye aikoni ya penseli chini ya jina la wasifu.
Ukiwa kwenye menyu ya Mipangilio unaweza:
- Kubadilisha ishara ya wasifu
- Kubadilisha jina la wasifu
- Kubadilisha lugha ya kuonyesha ya wasifu
- Kuweka Vidhibiti vya Wazazi
- Kuweka mapendeleo ya kucheza kiotomatiki kwa muhtasari na video zinazofuata
- Kufuta wasifu