Unaweza kuboresha utazamaji wako wa Showmax kwa kubadilisha upendavyo mipangilio ya manukuu ili kukidhi mahitaji yako. Fuata hatua hizi:
- Nenda kwenye Showmax.com kisha uingie kwenye akaunti.
- Nenda kwenye Akaunti kupitia upau wa menyu wa juu kulia.
- Chagua Mipangilio.
- chini hadi upate Mwonekano wa Manukuu na uchague Badilisha upendavyo.
- Badilisha upendavyo mwonekano wa manukuu kwa kurekebisha sehemu zozote kati ya zifuatazo:
- Ukubwa wa maandishi
- Muundo wa fonti
- Rangi ya Dirisha au Mandharinyuma
- Muundo na rangi ya kivuli
- Hifadhi mapendeleo yako ya manukuu kwa kubofya Hifadhi Mipangilio.
Ili kupata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha lugha ya manukuu yako, angalia Ninawashaje manukuu?
Muhimu:
Mwonekano wa sasa wa manukuu unaweza kubadilishwa mtandaoni pekee kwenye Showmax.com.