Sera ya Faragha ya Showmax
1. UTANGULIZI
1.1 Katika Showmax, tunajua kuwa faragha yako ni suala nyeti. Tunahitaji kuhakikisha kuwa data yako binafsi inatumika kisheria na ipasavyo, kwa lengo kuu la kuboresha huduma zetu na hali yako ya utazamaji.
1.2 Sera hii ya Faragha inaeleza jinsi data yako binafsi inavyochakatwa katika Showmax unapotumia tovuti, programu (ikiwa ni pamoja na Programu ya Showmax), bidhaa, mifumo na huduma zetu ili kuvinjari au kufikia maudhui, ikiwa ni pamoja na wakati ambapo hujasajiliwa au hujaingia katika huduma yetu. Hapa, tunaeleza pia baadhi ya njia unazoweza kutumia kudhibiti data yako binafsi, na kuwasiliana nasi iwapo una maswali yoyote. Data yako binafsi itachakatwa na Showmax kulingana na Sheria za Faragha zinazotumika katika nchi unakoishi.
1.3 Kulingana na nchi unakoishi na Huduma husika ya Showmax, mdhibiti wa data yako binafsi ni shirika lifuatalo la Showmax, ambapo kila moja limerejelewa hapa kama “Showmax”:
1.3.1 Iwapo unaishi nchini Afrika Kusini au Lesotho, mdhibiti wa data yako binafsi ni kampuni ya Showmax SA Proprietary Limited (namba ya usajili ya kampuni: 2022/672391/07), kampuni iliyosajiliwa kisheria na kupewa leseni ya kuhudumu kulingana na sheria za Jamhuri ya Afrika Kusini, iliyoko: 144 Bram Fischer Drive, Randburg, Johannesburg, Gauteng, 2194, Afrika Kusini.
1.3.2 Iwapo unaishi nchini Nigeria, mdhibiti wa data yako binafsi ni kampuni ya MSAT Nigeria Limited (namba ya usajili ya kampuni: RC 480418), kampuni iliyosajiliwa kisheria na kuidhinishwa kulingana na sheria za Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria iliyoko: Plot 1381 Tiamiyu Savage Street, Victoria Island, Lagos, Nigeria.
1.3.3 Iwapo unaishi katika moja ya nchi zilizotajwa hapa chini, mdhibiti wa data yako binafsi ni kampuni ya Showmax Africa Holdings Limited (namba ya usajili ya kampuni: 14402312), kampuni iliyosajiliwa kisheria na kuidhinishwa kulingana na sheria za Uingereza na Wales, iliyoko: 27 Old Gloucester Street, London, Uingereza, WC1N 3AX, Uingereza.
Angola, Benin, Botswana, Bukinafaso, Kameruni, Kepuvede, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Komoro, Kongo, Kodivua, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jibuti, Ginekweta (Equatorial Guinea), Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Gine, Ginebissau, Kenya, Madagaska, Malawi, Mali, Mauritania, Morisi (Mauritius), Msumbuji, Namibia, Nija, Rwanda, Saotome na Principe, Senegali, Ushelisheli (Seychelles), Sieraleoni, Tanzania, Togo, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
1.3.4 Kampuni hizi za Showmax Group zilizotajwa katika kifungu cha 1.3 ni washirika wa MultiChoice Group Limited, kampuni iliyoidhinishwa kuhudumu katika Jamhuri ya Afrika Kusini (namba ya usajili 2018/473845/06), ambayo ofisi yake iliyosajiliwa inapatikana katika MultiChoice City, 144 Bram Fischer Drive, Ferndale, Randburg, Gauteng, 2914, Jamhuri ya Afrika Kusini. Hivyo, MultiChoice Group of Companies ni Washirika wa Showmax Group.
1.3.5 Tunakuhimiza usome sera hii yote ili uelewe jinsi tunavyotegemea data binafsi kukutayarishia hali bora zaidi ya utumiaji. Tunatumia pia sera hii kukufahamisha kuhusu Vidakuzi vinavyosaidia kuendesha huduma zetu kwa upande wa kiufundi.
1.3.6 Ukiwa na maswali yoyote kuhusu jinsi Showmax inavyochakata data binafsi, unaweza kuwasiliana na afisa wetu wa ulinzi wa data katika dpo@showmax.com.
1.3.7 Isipokuwa ibainishwe vinginevyo, maneno yaliyofafanuliwa yana maana yaliyopewa katika Vigezo na Masharti ya Showmax yanayopatikana katika https://showmax.com/terms.
2. NI DATA GANI BINAFSI TUNAYOKUSANYA?
2.1 Muhtasari: Tunaweza kupokea na kukusanya taarifa zako binafsi kwa njia mbalimbali, kama vile unapopakua App ya Showmax kwenye kifaa chako; kujisajili kutumia Showmax; kutazama, kupakua, au kutumia huduma au maudhui yoyote ya Showmax (ikiwemo kuchagua maudhui unayopendelea), unapotoa taarifa za malipo, kuwasiliana na kituo chetu cha msaada, kushiriki katika shughuli za masoko au matangazo, au unapowasilisha taarifa zako binafsi kwetu kwa sababu nyingine yoyote.
2.2 Tunaweza pia kupokea data binafsi kutoka kwa washirika wengine ambao wameipata kutoka kwako na ambao wameruhusiwa kutupatia.
2.3 Aina za data binafsi ukiwa umeingia katika Akaunti yako ya Showmax: Aina za data binafsi ya watumiaji walioingia katika akaunti tunayokusanya inajumuisha:
2.3.1 Maelezo ya Kujisajili na Akaunti ya Showmax: Unapojisajili, ni lazima uweke jina lako na jina la ukoo, anwani ya barua pepe, namba ya simu ya mkononi na nenosiri ili kufungua Akaunti yako ya Showmax. Tutachakata pia maelezo unayoweka katika Akaunti yako ya Showmax, ikiwa ni pamoja na mapendeleo ya matangazo na mipangilio mingine;
2.3.2 Maelezo ya usajili na kulipa: Tunachakata maelezo kuhusu Mipango ya Usajili wako na muda wake. Kuhusiana na malipo yako ya Mipango ya Usajili, tunakusanya pia maelezo ya njia ya kulipa, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu maelezo fulani kuhusu kadi za mikopo na benki, pointi za uaminifu na vocha. Ukichagua kulipa kupitia njia ya kulipa ya mshirika mwingine, tunaweza pia kuchakata maelezo kuhusu malipo hayo na akaunti yako uliyofungua na mshirika huyo mwingine;
2.3.3 Historia na mapendeleo ya utazamaji: Tunakusanya maelezo kuhusu Maudhui unayotazama au kutumia, ikiwa ni pamoja na klipu au vionjo, maoni kuhusu maudhui, ikiwa yapo, na orodha za kutazama, kwa mfano filamu/vipindi na aina, utafutaji, muda na idadi ya vipindi vya kutazama, faili unazopakua, utazamaji na ubora wa faili ya kupakua. Kulingana na maelezo kuhusu Maudhui unayotazama, tunaweza kufahamu baadhi ya data inayokuhusu, k.m., mapendeleo ya maudhui yanayokuvutia kulingana na Maudhui unayochagua;
2.3.4 Matukio: Tunakusanya taarifa fulani kuhusu shughuli zako tunazoziona unapofikia na kutumia Tovuti ya Showmax, App ya Showmax, au unapojibu mawasiliano yetu ya masoko. Hii inajumuisha maelezo ya jinsi, lini, na kwa muda gani umepata, kutazama, au kutumia majukwaa yetu, pamoja na taarifa kuhusu trafiki ya tovuti na jinsi unavyotumia huduma (kwa mfano, maswali ya utafutaji, mwenendo wa kuvinjari, na muda wa kutazama). Ikiwa imewezeshwa, tunakusanya pia amri za sauti zinazosindika kupitia App ya Showmax.
2.3.5 Maelezo ya huduma ya usaidizi: Tunakusanya maelezo fulani kuhusu mawasiliano yako na kituo cha usaidizi cha Showmax (iwapo tunaweza kuhusisha mawasiliano hayo nawe), kama vile tarehe, saa na sababu ya kuwasiliana na Showmax, manukuu ya gumzo, barua pepe au mazungumzo mengine;
2.3.6 Vidakuzi: Tunaweza pia kuhifadhi maelezo fulani yanayokusanywa kupitia utumiaji wa vidakuzi, violezo vya wavuti, vitambulisho vya matangazo na teknolojia zingine, ikiwa ni pamoja na data ya matangazo. Ili upate maelezo zaidi kuhusu vidakuzi, rejelea sehemu ya Vidakuzi ya Sera hii ya Faragha;
2.3.7 Maelezo ya Kifaa na Kivinjari: Unapotumia Tovuti ya Showmax au Programu ya Showmax, tunaweza pia kukusanya maelezo kuhusu kifaa au kivinjari kinachotumika kufikia Huduma za Showmax, kama vile vitambulisho maalum vya kifaa, anwani ya IP, aina, muundo, mipangilio, mfumo wa uendeshaji, shughuli kwenye mfumo, lugha na ripoti za matukio ya kuacha kufanya kazi;
Unapofikia Tovuti ya Showmax au App ya Showmax, tunaweza pia kukusanya taarifa kuhusu kifaa au kivinjari unachotumia kufikia huduma za Showmax, kama vile kitambulisho cha kipekee cha kifaa, anwani ya IP, aina, muundo, mipangilio, mfumo wa uendeshaji, shughuli za mfumo, lugha, na ripoti za matatizo yanayotokea.
2.3.8 Maelezo ya Mahali: Unapotumia Tovuti ya Showmax au Programu ya Showmax, tunatambua mahali kilipo kifaa kinachotumika kufikia Huduma ya Showmax kulingana na anwani yako ya IP au benki inayotoa huduma ya njia yako ya kulipa. Showmax haitumii data ya mahali ya GPS na haikusanyi data ya mahali, hivyo kifungu 8.2.2 cha Makubaliano ya Leseni hakitumiki;
2.3.9 Maelezo ya Utafiti wa Mtumiaji: Tunakusanya maelezo fulani kuhusu kushiriki kwako katika Tafiti za Watumiaji wa Showmax (iwapo utaamua kuchangia, ambayo ni hiari yako kabisa), kama vile ukadiriaji wako wa vipengele mbalimbali vya Huduma ya Showmax, mapendeleo yako kuhusu vipengele vya Huduma ya Showmax na maoni na majibu yako kuhusu maswali fulani yanayohusiana na Huduma ya Showmax;
2.3.10 Maelezo unayotupatia kwenye mitandao ya kijamii: Ukiwasiliana nasi kupitia akaunti zetu za mitandao ya kijamii au ukijiunga katika shindano tunalopanga, tutachakata maelezo yanayopatikana katika akaunti yako ya mitandao ya kijamii, hasa, jina lako, jina la ukoo na anwani ya barua pepe, na maelezo mengine yoyote unayotupatia kwa hiari yako.
2.4 Aina za data ukiwa hujaingia katika Huduma ya Showmax: Aina za data binafsi tunazoweza kukusanya unapotumia Tovuti ya Showmax au Programu ya Showmax bila kuingia katika akaunti, inajumuisha data inayorejelewa katika sehemu zifuatazo: Matukio (2.2.4), Vidakuzi (2.2.6), Maelezo ya Kifaa na Kivinjari (2.2.7) na Maelezo ya Mahali (2.2.8).
2.5 Data ya wasifu: Tunaruhusu uundaji wa wasifu zinazoweza kuunganishwa na Akaunti moja ya Showmax, ambapo Watumiaji tofauti Walioidhinishwa (kama vile wanafamilia au familia) wanaweza kuunda wasifu wao binafsi na kuweka mapendeleo binafsi tofauti na yaliyokabidhiwa kwa wasifu mkuu na wasifu zingine zilizounganishwa na Akaunti moja kuu ya Showmax. Tunachakata jina la wasifu husika (huenda likawa au lisiwe jina la kwanza la mtu) na historia yake ya Utazamaji (2.2.3).
2.6 Data ya watoto: Lazima uwe na umri wa angalau miaka 18 au zaidi ili uweze kufungua Akaunti ya Showmax. Ingawa watu wenye umri wa chini ya miaka 18 wanaweza kutumia Huduma ya Showmax, wanaweza kuitumia tu chini ya usimamizi wa mzazi au mlezi. Inawezekana kuunda wasifu wa mtoto uliotengewa mtoto kwa kuweka Mipaka ya Umri inayofaa katika mipangilio ya wasifu. Hii itahakikisha kuwa uchezaji wa video za Maudhui yaliyokadiriwa kuwa juu ya Mipaka ya Umri iliyowekwa katika wasifu hazichezwi. Tunachakata jina la wasifu wa mtoto (huenda likawa au lisiwe jina la kwanza la mtoto) na historia yake ya Utazamaji (2.2.3).
2.7 Utoaji wa data kwa hiari: Ni hiari yako kutoa data yako binafsi lakini inahitajika ili kutumia baadhi ya huduma zinazotolewa na Showmax. Ukikataa kutoa baadhi ya data yako binafsi, itafanya iwe vigumu kutumia Huduma ya Showmax au baadhi ya vipengele vyake, kwa mfano, tovuti, programu, bidhaa, mifumo na huduma zake ili kuvinjari au kufikia maudhui, na itazuia Showmax kutoa na kutekeleza huduma hizo.
3. TUNACHAKATA DATA BINAFSI KWA MAKUSUDI GANI?
3.1 Muhtasari: Kwa kawaida tunatumia data binafsi tunayopokea na kukusanya kwa makusudi ya kutoa, kutangaza, kutunza, kuweka mapendeleo na kuboresha huduma zetu, kubuni huduma mpya na kulinda Showmax, mifumo yetu, washirika wa maudhui na watumiaji wetu kutokana na udanganyifu au shughuli ya kinyume cha sheria.
3.2 Makusudi: Tunachakata data yako binafsi kwa makusudi maalum ambayo yanajumuisha:
3.2.1 kuchakata data inayohitajika kwa makusudi ya uhitimishaji na utendaji wa makubaliano yetu nawe, ikiwa ni pamoja na:
3.2.1.1 kufungua na kutunza Akaunti yako ya Showmax ili kuthibitisha utambulisho wako unapoingia katika akaunti yako ya Showmax, kukuruhusu ufikie Maudhui kulingana na Mipango yako ya Usajili na kukamilisha malipo ya Mipango yako ya Usajili;
3.2.1.2 kukupa huduma ya Programu ya Showmax na vipengele vyake vyote, ikiwa ni pamoja na kipengele chake cha kutafuta kwa kutamka, iiwapo kinapatikana; na,
3.2.1.3 kukufahamisha kuhusu mabadiliko muhimu katika Makubaliano kati yako na Showmax, ikiwa ni pamoja na maelezo kuhusu masasisho ya Vigezo na Masharti na taarifa nyingine muhimu.
3.2.2 kuelewa mambo yanayokuvutia na kuboresha hali ya utazamaji ili ikufae na kukupa mapendekezo yanayohusiana ya chaguo la kipekee la filamu/vipindi vilivyochaguliwa kimahususi kwa ajili yako kulingana na mapendeleo na historia yako ya Utazamaji (2.2.3); uchakataji wa data yako binafsi kwa kusudi hili unalingana na maslahi yetu ya kisheria;
3.2.3 kutoa huduma za usaidizi kwa wateja na kuwasiliana nawe, ikiwa ni pamoja na kupitia mitandao ya kijamii, na kukufahamisha kuhusu mabadiliko yoyote katika bidhaa na huduma za Showmax; uchakataji wa data yako binafsi kwa kusudi hili unalingana na maslahi yetu ya kisheria;
3.2.4 uchakataji wa data binafsi ili kutimiza wajibu mwingine unaotokana na masharti ya sheria zinazotumika, k.m., katika sehemu ya uhasibu na malipo ya kodi;
3.2.5 kutimiza wajibu wowote wa kimkataba kwa washirika wetu wa biashara kwa kusudi la kutoa bidhaa na huduma za Showmax na kwa makusudi ya ukamilishaji wa malipo yanayohusika; uchakataji wa data yako binafsi kwa kusudi hili unalingana na maslahi yetu ya kisheria;
3.2.6 uchakataji wa data binafsi kwa utangazaji wa Huduma ya Showmax au bidhaa au huduma za Makampuni Washirika (ambayo itamaanisha katika Sera hii ya Faragha kuwa, anayedhibitiwa na Showmax; (ii) aliye chini ya udhibiti wa pamoja na Showmax, (iii) anayedhibiti Showmax; (iv) ambaye anashirikiana na Showmax au watu wowote waliodhaniwa (i), (ii) au (iii) aliyeweka mkataba wa ushirikiano au biashara ya pamoja (“Mshirika wa JV”); (v) anayedhibitiwa na, au aliye chini ya udhibiti wa pamoja na, Mshirika yeyote wa JV; na (iv) makampuni yote tanzu yanayoshirikiana moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na kampuni ya MultiChoice Group Limited. Hii inajumuisha matangazo ya moja kwa moja na matangazo ya kulengwa kulingana na mapendeleo na utumiaji wako wa Huduma ya Showmax (yaani, matangazo yanayolingana na mambo yanayokuvutia). Uchakataji wa data yako binafsi kwa kusudi hili unalingana na maslahi yetu/ya Kampuni Mshirika inayohusika ya kisheria, au panapohitajika, kulingana na idhini yako. Katika mipangilio ya Akaunti yako ya Showmax, unaweza (i) kudhibiti mapendeleo yako ya matangazo au kujiondoa ili usipokee mawasiliano ya matangazo kwa kutumia njia zilizowekwa katika kila mawasiliano unayopokea (k.m., kiungo cha kujiondoa), na (ii) jiondoe usipokee matangazo yanayolingana mambo yanayokuvutia.
3.2.7 uchakataji kwa makusudi ya utafiti, majaribio, takwimu, ubunifu, uboreshaji (ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa hali ya utumiaji na utafiti wa soko), usimamizi, utunzaji, usaidizi wa kifundi na usalama wa Huduma ya Showmax, Tovuti ya Showmax na Programu ya Showmax, bidhaa na huduma za Makampuni Washirika na teknolojia ya mshirika mwingine inayotolewa na watoa huduma wetu. Tunaweza (na kila Kampuni Mshirika) pia kuchakata data yako binafsi ili kubuni bidhaa na huduma mpya, na uchakataji wa data yako binafsi kwa kusudi hili unalingana na maslahi yetu/ya Kampuni Mshirika inayohusika ya kisheria, na haki yako ya kupinga uchakataji huo;
3.2.8 uchakataji kwa makusudi ya kuchunguza, kutekeleza na kutetea madai ya kisheria, kutekeleza au kuchunguza ukiukaji unaoweza kutokea wa masharti yetu ya utumiaji au shughuli zingine zozote halisi au zinazodaiwa za udanganyifu (ikiwa ni pamoja na ukiukaji wa hakimiliki), kulinda haki, mali au usalama wa Showmax, wateja wetu, wafanyakazi na washirika wengine; uchakataji wa data yako binafsi kwa kusudi hili unalingana na maslahi yetu ya kisheria; na
3.2.9 Uchakataji kwa makusudi ya kupanga upya kikundi cha Showmax, ikiwa ni pamoja na mabadiliko katika umiliki au udhibiti wa mali, hisa au usimamizi wa Showmax, au wa Makampuni zetu Washirika; uchakataji wa data yako binafsi kwa kusudi hili unalingana na maslahi yetu ya kisheria.
4. NI NANI WANAOPOKEA DATA BINAFSI
4.1 Data yako binafsi inaweza kutolewa kwa aina zifuatazo za wapokeaji:
4.1.1 Makampuni Washirika, ambayo inajumuisha makampuni zetu kuu, makampuni tanzu na mashirika yanayodhibiti au yaliyo chini ya udhibiti wa pamoja na Showmax, hasa inapohitajika kwa matengenezo ya mara kwa mara na kuendelea kukupa Huduma ya Showmax;
4.1.2 watoa huduma wanaoaminika tunaoshirikiana nao ili kuboresha au kukupa Huduma ya Showmax, wanaotenda kulingana na maagizo yetu, ikiwa ni pamoja na watoa huduma za upangishaji, utoaji wa huduma ya mfumo, uboreshaji na matengenezo, watoa huduma za usaidizi na usalama, watoa huduma za malipo na upatanisho;
4.1.3 watoa huduma za utangazaji wanaotusaidia katika kutangaza Huduma ya Showmax, ikiwa ni pamoja na mashirika ya utangazaji, usambazaji wa barua pepe na watoa huduma wengine wa zana za utangazaji, pamoja na watoa huduma za takwimu;
4.1.4 washirika wanaoweza kutoa huduma ya mipango ya usajili katika Huduma ya Showmax kwa niaba yetu na/au washirika ambao Showmax inashirikiana nao ili kuweka bidhaa za Showmax kwenye mifumo yao;
4.1.5 washirika wengine, ikiwa ni pamoja na mashirika ya serikali, mahakama au mashirika kama hayo, inapohitajika ili kutii sheria zinazotumika, kutekeleza au kuchunguza uwezekano wa kufanyika kwa shughuli za ukiukaji wa masharti yetu ya utumiaji au mkataba mwingine wowote kati yako nasi, kulinda haki, mali au usalama wetu au wa wateja, wafanyakazi na washirika wengine wowote; na/au
4.1.6 mshirika mwingine kuhusiana na kupangwa upya kwa kikundi cha Showmax, kimahususi, mshirika mwingine anayenunua (au kupendekeza kununua) umiliki au udhibiti wa mali zetu, hisa au usimamizi, au wa Makampuni zetu Washirika kwa njia yoyote, au mshirika mwingine tunayenunua kwake umiliki au udhibiti wa mali, hisa au usimamizi.
4.2 Iwapo data binafsi itahamishwa kwenda nje ya nchi, Showmax huchukua hatua zinazohitajika kisheria kulingana na Sheria za Faragha zinazotumika ili kuhakikisha kuwa data binafsi inalindwa ipasavyo katika nchi hizo, kimahususi, kwa kuweka makubaliano na wapokeaji husika wa data kuhusu kiwango cha juu zaidi cha ulinzi wa data.
5. HAKI ZAKO NI ZIPI?
5.1 Haki zako kama mmiliki wa data. Una haki zifuatazo kuhusiana na data yako binafsi inayochakatwa na Showmax:
5.1.1 Ufikiaji: Una haki ya kufikia data yako binafsi. Ili uombe kufikia data yako binafsi, tafadhali tembelea Tovuti yetu ya Faragha
5.1.2 Urekebishaji: Unaweza kutuomba turekebishe data binafsi isiyo sahihi. Unaweza kubadilisha mwenyewe maelezo ya msingi yanayokuhusu katika mipangilio ya Akaunti yako ya Showmax. Tafadhali kumbuka kuwa ukiwasha kipengele cha usalama wa hali ya juu katika Akaunti yako ya Showmax, utatakiwa kuthibitisha utambulisho wako kabla ya kuona au kubadilisha data yako binafsi. Kwa maombi mengine ya urekebishaji, tafadhali wasiliana nasi kupitia dpo@showmax.com.
5.1.3 Ufutaji: Unaweza kutuomba tufute data binafsi. Ili uombe ufutaji wa data yako binafsi, tafadhali tembelea Tovuti yetu ya Faragha. Tafadhali kumbuka ombi lako la ufutaji litasababisha kukatishwa kwa usajili wako na utafahamishwa mapema. Kiwango ambacho tunaweza kutii ombi lako la ufutaji wa data binafsi kinaweza kuthibitiwa na wajibu wetu wa kisheria wa kuhifadhi baadhi ya data binafsi. Tunaweza pia kuhifadhi data binafsi inayohitajika katika uthibitishaji, utekelezaji au uteteaji wa madai yetu ya kisheria.
5.1.4 Kukataa kupokea matangazo: Katika mipangilio ya Akaunti yako ya Showmax, tunakupa uwezo wa kuonyesha mapendeleo yako kuhusiana na kupokea mawasiliano ya matangazo kutoka Showmax. Unaweza pia kujiondoa ili usipokee mawasiliano ya matangazo kwa kutumia njia zilizowekwa katika kila mawasiliano unayopokea (k.m., kiungo cha kujiondoa). Tafadhali kumbuka kuwa inaweza kuchukua siku kadhaa kwa ombi hili kushughulikiwa. Huwezi kujiondoa ili usipokee mawasiliano yanayohusiana na malipo au usimamizi wa huduma. Vilevile, unaweza kujiondoa ili usipokee matangazo yanayolingana na mambo yanayokuvutia. Unaweza pia kudhibiti mapendeleo yako kuhusu matumizi ya vidakuzi na utoaji wa data yako kwa washirika wetu wanaoaminika kwa makusudi ya matangazo na utangazaji.
5.1.5 Kupinga uchakataji mwingine: Unaweza kupinga uchakataji wa data yako binafsi kulingana na maslahi ya kisheria ya Showmax isipokuwa tuwe na sababu nzuri ya kuendelea kuchakata data hiyo. Katika mipangilio ya Akaunti yako ya Showmax, unaweza kujiondoa ili data ya takwimu na data kutoka katika akaunti yako isichakatwe kwa kusudi la kuboresha bidhaa na huduma za Showmax. Iwapo ungependa kupinga uchakataji mwingine wowote kulingana na maslahi yetu ya kisheria, tafadhali tuma ombi lako kupitia dpo@showmax.com.
5.1.6 Uwezo wa kuhamishwa: Unaweza kutuomba tupokee data yako binafsi uliyowasilisha katika Showmax katika muundo unaoweza kusomeka na mashine au kutaka data hiyo ihamishiwe kwa mshirika mwingine. Ili uombe data yako binafsi ihamishwe, tafadhali tembelea Tovuti yetu ya Faragha.
5.1.7 Uzuiaji: Unaweza pia kuomba tuzuie uchakataji wa data yako binafsi, hasa iwapo unaamini kwua uchakataji huo ni kinyume cha sheria au data yako si sahihi. Ili uombe uzuiaji wa uchakataji, tafadhali tembelea dpo@showmax.com.
5.2 Uondoaji wa idhini. Wakati mwingine, tunaweza kuomba idhini yako ya uchakataji. Katika hali hizo, una haki ya kuondoa idhini yako wakati wowote, bila kuathiri uhalali wa uchakataji unaotokana na idhini kabla haijaondolewa.
5.3 Tunaweza kukuomba maelezo ya ziada ili tuweze kukutambua, ikiwa ni pamoja na uthibitisho wa utambulisho.
5.5 Malalamiko: Unaweza kuwasilisha malalamiko kuhusu uchakataji wetu wa data kwa msimamizi wa ulinzi wa data wa mahali ulipo. Iwapo utatatizika kuwasiliana na msimamizi wa ulinzi wa data, tutakusaidia. Tafadhali wasiliana nasi kupitia dpo@showmax.com kwa kusudi hili.
6. TUNAHIFADHI KWA MUDA GANI?
6.1 Kanuni ya Uhifadhi wa Data: Tunachakata data yako binafsi unapojisajili na baada ya kukamilika kwa usajili wako kwa muda ambao data hiyo inahitajika kwa makusudi tunayoruhusiwa na/au tunayohitajika kuchakata data hiyo, ikiwa ni pamoja na kwa makusudi yafuatayo:
6.1.1 kutii wajibu wa Showmax unaotokana na sheria zinazotumika;
6.1.2 kuthibitisha, kutekeleza au kutetea madai ya kisheria, pamoja na kwa makusudi ya kesi nyingine zozote za kisheria au utiifu wa hukumu na/au maamuzi yoyote yaliyotolewa na mamlaka za umma;
6.1.3 utafiti na takwimu; na
6.1.4 utangazaji wa bidhaa na huduma za Showmax.
6.2 Kanuni za uhifadhi wa data kuhusiana na idhini: Kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 5.2, tunaweza kuchakata data yako kutokana na idhini. Katika tukio hilo, tutachakata data mradi tu idhini inatumika na kwa muda ambao data hiyo inahitajika kwa makusudi tunayoruhusiwa na/au tunayohitajika kuchakata data hiyo.
6.3 Panapofaa, tutasimba kwa njia fiche, kuficha utambulisho wa data, kuondoa maelezo ya utambulisho na/au kutenganisha maelezo ili tuweze kuyatumia kwa namna inayoepuka kutambulishwa kiholela, kwa maslahi ya kulinda faragha yako na kuimarisha mbinu za usalama.
7. USALAMA
Kudumisha usalama na ukamilifu wa data yako binafsi ni suala tunalolipa kipaumbele cha juu na tunajitahidi kuweka mbinu zinazofaa za kiufundi na kishirika ili kulinda uadilifu wa maelezo, kwa kutumia viwango vya teknolojia vinavyokubalika ili kuzuia kufikiwa au kutolewa kwa data yako binafsi bila idhini na kuilinda kutokana na kutumiwa vibaya, kupotea, kubadilishwa au kuharibiwa.
8. VIDAKUZI
8.1 Ili kuhakikisha kuwa Tovuti ya Showmax, Programu ya Showmax na Huduma ya Showmax vinafanya kazi vizuri, ili kukupa hali ya utumiaji inayokufaa, sisi na watoa huduma wetu wengine tunaweza kuweka vidakuzi au teknolojia kama hiyo kama vile hasa violezo vya wavuti, SDK, pikseli na vitambulisho vya utangazaji (vinavyorejelea hapa kwa pamoja kama “vidakuzi”) kwenye kifaa chako, kwa kutegemea idhini yako panapohusika. Kidakuzi ni faili ndogo ya maandishi ambayo tovuti huhifadhi kwenye kompyuta au kifaa chako cha mkononi unapotembelea tovuti. Inawezesha tovuti kukumbuka vitendo na mapendeleo yako (kama vile hali ya kipindi, lugha, ukubwa wa fonti na mapendeleo mengine ya onyesho) kwa muda, ili usihitaji kuviweka kila mara unaporejea kwenye tovuti au kuvinjari kutoka ukurasa mmoja hadi mwingine.
8.2 Tovuti ya Showmax hutumia vidakuzi viwili vya msingi: vidakuzi vya kipindi na vidakuzi vya kudumu. Vidakuzi vya kipindi ni faili za muda zinazohifadhiwa kwenye kifaa cha mtumiaji hadi mtumiaji atakapoondoka kwenye kifaa, atkapoondoka kwenye tovuti au atakapofunga programu (kivinjari). Vidakuzi vya kudumu huhifadhiwa kwenye kifaa cha mtumiaji kwa muda uliowekwa katika mipangilio ya vidakuzi au hadi vitakapofutwa na mtumiaji. Vidakuzi vyote vya kudumu hufutwa katika kipindi cha miezi 13 kuanzia wakati vilipohifadhiwa kwenye kifaa.
8.3 Katika hali nyingi, mipangilio chaguomsingi ya programu ya kuvinjari (kivinjari) huwezesha kuhifadhi vidakuzi kwenye kifaa cha mtumiaji. Unaweza kufuta au kuzuia vidakuzi visiwekwe katika mipangilio ya kivinjari chako au programu inayohusika. Vidakuzi vinavyowekwa na Showmax vinaweza kubainishwa kama vidakuzi vya mshirika mkuu, na vile vinavyowekwa na washirika wetu vitabainishwa kama vidakuzi vya mshirika mwingine. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu washirika wetu ambao wanaruhusiwa kufikia data inayokusanywa na vidakuzi kwa kubofya kiungo cha Mapendeleo ya Vidakuzi kilichojumuishwa katika kijachini kinachofaa cha Tovuti ya Showmax au mipangilio ya Akaunti yako ya Showmax. Sehemu fulani za Tovuti ya Showmax, Huduma ya Showmax au Programu ya Showmax huenda isifanye kazi vizuri ikiwa vidakuzi vya mshirika mkuu vitazuiwa au kufutwa.
8.4 Aina ya vidakuzi na makusudi ya kutumika kwake kwenye Tovuti ya Showmax na Programu ya Showmax inajumuisha:
8.4.1 Vidakuzi vya lazima, ambavyo vinahitajika kwa utendakazi wa Huduma ya Showmax, ikiwa ni pamoja na usalama na uzuiaji wa udanganyifu, na kuwezesha utaratibu wa ununuzi. Kutumika kwa vidakuzi hivi hakuhitaji idhini yako. Ukiweka mipangilio ya kuzuia vidakuzi hivi kwenye kivinjari chako, baadhi ya sehemu za Huduma ya Showmax huenda zisifanye kazi vizuri.
8.4.2 Vidakuzi vya kuhakikisha usalama, kuzuia udanganyifu na utatuzi wa hitilafu ambavyo vinatusaidia kufuatilia na kuzuia shughuli za udanganyifu na kuhakikisha kuwa mifumo na taratibu zinafanya kazi vizuri na kwa usalama. Kutumika kwa vidakuzi hivi hakuhitaji idhini yako.
8.4.3 Vidakuzi vya kuhifadhi na/au kufikia maelezo kwenye kifaa, ambavyo vinatusaidia sisi na washirika wetu kuhifadhi au kufikia vidakuzi, vitambulisho vya kifaa au maelezo mengine kwenye kifaa chako. Kutumika kwa vidakuzi hivi kunategemea idhini yako.
8.4.4 Vidakuzi vya matangazo na maudhui yaliyoboreshwa ili kukufaa, vipimo, maarifa kuhusu hadhira na ubunifu wa bidhaa. Kutumika kwa vidakuzi hivi kunategemea idhini yako. Unaweza kuchagua kuidhinisha aina ndogo mahususi za makusudi, ikiwa ni pamoja na (i) kuonyesha matangazo kwenye tovuti za washirika wengine kulingana na maudhui unayotazama, programu unayotumia, eneo unalokadiriwa kuwa, au aina ya kifaa chako (matangazo ya kawaida), (ii) kutayarisha wasifu unaokuhusu na mambo yanayokuvutia kwa makusudi ya kukupendekezea Maudhui yanayokufaa, (iii) kupendekeza Maudhui kulingana wasifu uliyotayarishwa kukuhusu, (iv) kutayarisha wasifu unaokuhusu na mambo yanayokuvutia kwa kusudi la kukuonyesha matangazo yanayokufaa, (v) kuonyesha matangazo yanayokufaa kulingana na wasifu uliyotayarishwa kukuhusu (vi) kupima utendaji na ubora wa Maudhui unayotazama au kutumia, (vii) kupima ubora wa utendaji wa matangazo, (viii) kufanya utafiti wa soko (ix) kubuni na kuboresha bidhaa zetu.
8.5 Utaweka mapendeleo yako ya vidakuzi utakapotembelea mara ya kwanza Tovuti ya Showmax, Huduma ya Showmax au Programu ya Showmax. Unaweza kudhibiti mapendeleo yako ya vidakuzi na vilevile kuondoa idhini yako wakati wowote kwa kubofya kiungo cha Mapendeleo ya Vidakuzi kilichojumuishwa katika kijachini kinachofaa cha Tovuti ya Showmax au mipangilio ya Akaunti yako ya Showmax.
9. MABADILIKO KATIKA SERA HII NA MASHARTI YA MWISHO
9.1 Tunaweza kubadilisha Sera hii ya Faragha mara kwa mara. Tukifanya mabadiliko, tutachapisha sera iliyorekebishwa katika Showmax na tutafahamisha wateja kuhusu marekebisho hayo na tarehe yatakapoanza kutumika.
9.2 Iwapo kutakuwa na tofauti kati ya Sera hii ya Faragha na Makubaliano ya Leseni, masharti ya Sera hii ya Faragha yatatumika.
9.3 Sera hii ya Faragha inaweza kutolewa katika lugha kadhaa. Iwapo kutakuwa na tofauti yoyote, toleo la Kiingereza litatumika.
9.4 Ikiwa una maswali yoyote kuhusu Sera hii ya Faragha au uchakataji wa data yako binafsi, tafadhali wasiliana nasi katika dpo@showmax.com.