VIGEZO NA MASHARTI YA SHOWMAX

Vigezo na masharti haya ya huduma ya Showmax yanatumika kwa matumizi ya huduma ya Showmax. Tafadhali soma vigezo na masharti haya kwa umakini.

1. HUDUMA YA SHOWMAX NA KUKUBALIANA KWAKO NA VIGEZO HIVI VYA SHOWMAX

1.1 Showmax ("Showmax" au “sisi” au “nasi” au "yetu”) hutoa huduma ya kutiritisha maudhui popote ulipo inayopatikana kwa namna mbalimbali ya Mipango ya Usajili wa Showmax (“Huduma ya Showmax”) ambayo inaweza kufikiwa kwenye tovuti https://showmax.com ambayo watumiaji wanaweza kuitumia kutiririsha au kupakua vipindi vya televisheni, filamu, matukio mubashara ya michezo, video au klipu za sauti na nyenzo nyingine za video, inavyohitajika (“Maudhui”) kwa kutumia kifaa cha kielektroniki kinachoweza kuunganishwa na mtandao, ikijumuisha kompyuta binafsi, simu za mkononi, tableti, vicheza faili za sauti na video, TV mahiri, ving'amuzi, kifaa cha michezo ya video na vifaa vingine kama hivyo, kama inavyoelezwa zaidi katika kifungu cha 6 cha vigezo na masharti haya ya Showmax (“Kifaa cha Kufikia”).

1.2 Huduma ya Showmax inatolewa na Showmax chini ya vigezo na masharti yaliyo kwenye tovuti https://showmax.com/terms/ (“Vigezo hivi vya Showmax”). Tafadhali kumbuka kuwa yafuatayo yamejumuishwa na yanaunda sehemu ya Vigezo na Masharti haya ya Showmax:

1.2.1 sera yetu ya faragha, inayopatikana katika https://showmax.com/privacy/ (“Sera ya Faragha”);

1.2.2 vigezo vya jumla vya utumiaji wa tovuti ya Showmax ambavyo vinapatikana katika https://showmax.com na URL nyingine kama hizo ambazo Showmax inaweza kutumia kutoa Huduma ya Showmax (“Tovuti ya Showmax”), zinazopatikana katika https://showmax.com/website-terms/ (“Vigezo vya Utumiaji wa Tovuti”); na

1.2.3 Makubaliano ya Leseni ya Mtumiaji wa Hatima wa Programu ya Showmax (“Makubaliano ya Leseni”), yanapatikana katika https://showmax.com/licence-agreement/.

1.3 Ukikubali Vigezo hivi vya Showmax, unakubali pia kufuata masharti ya Vigezo na Masharti, Vigezo vya Matumizi ya Tovuti na Makubaliano ya Leseni, kama kwamba vimejumuishwa kikamilifu katika Vigezo hivi vya Showmax.

1.4 Unapofungua akaunti yako, unatakiwa kukubali Vigezo vya Showmax. Huruhusiwi kutumia kwa namna yoyote Maudhui au Huduma ya Showmax ikiwa hukubali Vigezo hivi vya Showmax. Ukitumia kwa namna yoyote Maudhui au Huduma ya Showmax, hii itamaanisha kuwa unakubali Vigezo hivi vya Showmax. Ikiwa hukubali Vigezo hivi vya Showmax, lazima uache mara moja kutumia Maudhui na Huduma ya Showmax.

1.5 Vigezo hivi vya Showmax, ikiwa ni pamoja na hati zozote zilizorejelewa hapa, vinaunda makubaliano ya kisheria ya kuwajibisha kati ya Mteja na Showmax ("Makubaliano"). Makubaliano haya yataendelea kutumika hadi yatakapokomeshwa na Mteja au nasi katika moja ya njia zilizoelezwa katika Vigezo hivi vya Showmax.

1.6 Kulingana na mahali unapoishi, Huduma ya Showmax inatolewa kwako na shirika lifuatalo la Showmax:

1.6.1 Ikiwa unaishi nchini Afrika Kusini au Lesoto, Showmax inamaanisha shirika la Showmax SA Proprietary Limited (namba ya usajili ya kampuni: 2022/672391/07), kampuni iliyosajiliwa kisheria na kuidhinishwa kulingana na sheria za Jamhuri ya Afrika Kusini, iliyoko: 144 Bram Fischer Drive, Randburg, Johannesburg, Gauteng, 2194, Afrika Kusini.

1.6.2 Ikiwa unaishi nchini Naijeria, Showmax inamaanisha shirika la MSAT Nigeria Limited (namba ya usajili ya kampuni: RC 480418), kampuni iliyosajiliwa kisheria na kuidhinishwa kulingana na sheria za Shirikisho la Jamhuri ya Naijeria, iliyoko: Plot 1381 Tiamiyu Savage Street, Victoria Island, Lagos, Naijeria.

1.6.3 Ikiwa unaishi katika moja ya nchi zilizotajwa hapa chini, Showmax inamaanisha shirika la Showmax Africa Holdings Limited (namba ya usajili ya kampuni: 14402312), kampuni iliyosajiliwa kisheria na kuidhinishwa kulingana na sheria za Uingereza na Wales, iliyoko: 27 Old Gloucester Street, London, Uingereza, WC1N 3AX, Uingereza:

Angola, Benin, Botswana, Bukinafaso, Kameruni, Kepuvede, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Komoro, Kongo, Kodivua, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jibuti, Ginekweta (Equatorial Guinea), Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Gine, Ginebissau, Kenya, Madagaska, Malawi, Mali, Mauritania, Morisi (Mauritius), Msumbuji, Namibia, Nija, Rwanda, Saotome na Principe, Senegali, Ushelisheli (Seychelles), Sieraleoni, Tanzania, Togo, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

1.7 Sheria inayosimamia Vigezo vya Showmax na uhusiano wako na Showmax itabainishwa ifuatavyo:

1.7.1 Ikiwa unapata Huduma ya Showmax kupitia kampuni ya Showmax SA Proprietary Limited, Vigezo vya Showmax vitasimamiwa na sheria za Jamhuri ya Afrika Kusini.

1.7.2 Ikiwa unapata Huduma ya Showmax kupitia kampuni ya MSAT Nigeria Limited, Vigezo vya Showmax vitasimamiwa na sheria za Naijeria.

1.7.3 Ikiwa unapata Huduma ya Showmax kupitia kampuni ya Showmax Africa Holdings Limited, Vigezo vya Showmax vitasimamiwa na sheria za Uingereza na Wales.

1.8 Kampuni hizi za Showmax Group zilizotajwa katika kifungu cha 1.7 ni washirika wa MultiChoice Group Limited, kampuni iliyoidhinishwa kuhudumu katika Jamhuri ya Afrika Kusini (namba ya usajili 2018/473845/06), ambayo ofisi yake iliyosajiliwa inapatikana katika MultiChoice City, 144 Bram Fischer Drive, Ferndale, Randburg, Gauteng, 2914, Jamhuri ya Afrika Kusini.

2. MABADILIKO KATIKA VIGEZO VYA SHOWMAX

2.1 Tunaweza kubadilisha Vigezo vya Showmax wakati wowote. Ikiwa wewe ni Mteja, tutakufahamisha kuhusu mabadiliko hayo. Tutafanya hivyo kwa kukutumia barua pepe, SMS au kupitia njia zingine zilizoelezwa katika kifungu cha 20.3, ikiwa ni pamoja na taarifa ibukizi unapoingia katika akaunti tutakayokufungulia baada ya kujisajili ili kutumia Huduma ya Showmax (“Akaunti ya Showmax”), au kupitia programu tuliyosanidi au kutoa kwa watumiaji ili kufikia na kupokea Huduma ya Showmax (“Programu ya Showmax”). “Mteja” ni mtu ambaye amejisajili ili kutumia Huduma ya Showmax kupitia utaratibu wa kujisajili ulioidhinishwa na Showmax na amenunua angalau Mpango mmoja wa Usajili wa Huduma ya Showmax (ikiwa ni pamoja mpango wa Kujaribu Bila Malipo, ikiwa unapatikana), na usajili wake umekubalika na Showmax.

2.2 Ikiwa wewe si Mteja, mabadiliko yote katika Vigezo hivi vya Showmax yataanza kutumika kuanzia wakati tunapoyachapisha kwenye Tovuti ya Showmax. Ni jukumu lako kusoma na kupitia Vigezo hivi vya Showmax (ikiwa ni pamoja na mabadiliko yoyote katika Vigezo vya Showmax tunavyoweza kufanya) wakati wowote ukitaka kutumia Maudhui au Huduma ya Showmax.

2.3 Ukiendelea kutumia Huduma ya Showmax baada ya kufahamishwa kuhusu mabadiliko yoyote katika Vigezo vya Showmax, kama ilivyoelezwa hapo juu, unakubali toleo lililorekebishwa la Vigezo vya Showmax. Ikiwa hukubali mabadiliko yoyote katika Vigezo hivi vya Showmax, lazima uache kutumia Huduma ya Showmax kwa njia iliyoelezwa katika kifungu cha 14.1 hapa chini.

3. NI NINA ANAYEWEZA KUTUMIA HUDUMA YA SHOWMAX?

3.1 Unaweza tu kutumia Huduma ya Showmax ikiwa unatii Vigezo hivi vya Showmax na:

3.1.1 wewe ni Mteja; au

3.1.2 umeruhusiwa na Mteja kufikia au kutumia Huduma ya Showmax kupitia Akaunti ya Showmax ya Mteja (ikiwa ni pamoja na kupitia moja ya wasifu wake) (“Mteja Aliyeidhinishwa”). Ikiwa wewe ni Mtumiaji Aliyeidhinishwa, haki zako za kutumia Huduma ya Showmax zitakoma wakati haki za Mteja za kutumia Huduma ya Showmax zitakapokoma au Mteja atakapokoma kukuruhusu kufikia au kutumia Huduma ya Showmax kupitia Akaunti ya Showmax ya Mteja.

3.2 Mteja lazima ahakikishe kuwa Watumiaji wote Walioidhinishwa wanaofikia au kutumia Huduma ya Showmax kupitia Akaunti ya Showmax ya Mteja, wanafahamu Vigezo hivi vya Showmax, wanakubali Vigezo hivi vya Showmax na wanatii Vigezo hivi vya Showmax.

3.3 Vitendo vyote na kutotenda kwa Watumiaji Walioidhinishwa vitachukuliwa kama, na pia kuzingatiwa kuwa (i) vitendo na kutotenda kwa Mteja ambaye Akaunti yake ya Showmax imetumika kufikia au kutumia Huduma ya Showmax; na (ii) vitendo na kutotenda kwa Watumiaji wengine Walioidhinishwa wa Akaunti hiyo ya Showmax. Vitendo vyote na kutotenda kwa Mteja vitachukuliwa kama, na pia kuzingatiwa kuwa, vitendo na kutotenda kwa Watumiaji Walioidhinishwa wanaofikia au kutumia Huduma ya Showmax kupitia Akaunti ya Showmax ya Mteja. Kitendo au kutotenda inajumuisha ukiukaji wowote wa Vigezo hivi vya Showmax.

3.4 Lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi ili kujisajili katika Huduma ya Showmax na hupaswi kujaribu kujisajili katika Huduma ya Showmax ikiwa hujafikisha umri wa miaka 18 au zaidi.

3.5 Ikiwa Mtumiaji Aliyeidhinishwa hajafikisha umri wa 18, basi Mtumiaji huyo Aliyeidhinishwa lazima aruhusiwe na mzazi wake au mlezi rasmi kutumia Huduma ya Showmax na akubali Vigezo hivi vya Showmax na anapaswa tu kutumia Huduma ya Showmax chini ya usimamizi wa Mteja au Mtumiaji mwingine Aliyeidhinishwa aliyefikisha umri wa 18 au zaidi.

3.6 Tuna haki ya kukataa kukuruhusu ujisajili au kutumia Huduma ya Showmax kwa hiari yetu. Tunaweza kufanya hivyo hata kama utakamilisha utaratibu wa kujisajili na kukubali Vigezo hivi vya Showmax.

3.7 Hatulazimishwi kwa njia yoyote kutoa sababu ikiwa hatutakuruhusu ujisajili au kutumia Huduma ya Showmax.

4. TAARIFA NA MAELEZO YAKO

4.1 Maelezo yote unayotupatia lazima yawe ya kweli, sahihi na kamili. Hii inajumuisha jina lako na jina la ukoo, pamoja na anwani ya barua pepe na namba ya simu ya mkononi (“Maelezo ya Mawasiliano”) tunayokuomba utoe wakati wa utaratibu wa kujisajili na wakati wowote baadaye.

4.2 Lazima utufahamishe ikiwa maelezo uliyotupatia, ikijumuisha Maelezo ya Mawasiliano, yatabadilika au ikiwa si sahihi au si kamili. Usipotufahamisha, tutaendelea kutumia na kutegemea maelezo ya hivi karibuni zaidi uliyotupatia.

4.3 Mteja ataweza kubadilisha maelezo binafsi ya Mteja, ikijumuisha Maelezo ya Mawasiliano, kwa kuingia katika Akaunti ya Showmax ya Mteja kupitia Huduma ya Showmax au kwa kuwasiliana na mawakala wetu wa huduma ya usaidizi kwa wateja kwa kutumia maelezo ya mawasiliano yaliyotolewa katika kifungu cha 20.7. Tafadhali kumbuka kuwa tunaweza kuhitaji maelezo ya ziada kutoka kwako au kukuomba ujithibitishe kupitia njia zozote tunazoweza kutumia mara kwa mara, ili tuweze kukutambua kama Mteja.

4.4 Tafadhali pia soma Sera ya Faragha ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia maelezo yako na haki na wajibu wako.

4.5 Tunaweza kutuma data yako binafsi kwa Makampuni Washirika (ambayo itamaanisha katika Vigezo hivi vya Showmax kuwa, mtu mwingine yeyote (i) anayedhibitiwa na Showmax; (ii) aliye chini ya udhibiti wa pamoja na Showmax, (iii) anayedhibiti Showmax; (iv) ambaye anashirikiana na Showmax au watu wowote waliodhaniwa (i), (ii) au (iii) aliyeweka mkataba wa ushirikiano au biashara ya pamoja (“Mshirika wa JV”); (v) anayedhibitiwa na, au aliye chini ya udhibiti wa pamoja na, Mshirika yeyote wa JV; na (iv) makampuni yote tanzu yanayoshirikiana moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na kampuni ya MultiChoice Group Limited (“MultiChoice”), ili kukutangazia bidhaa za MultiChoice au Showmax au bidhaa au huduma zingine kwa kutegemea haki yako ya kukataa au kujiondoa katika huduma ya kupokea mawasiliano yoyote ya matangazo ya moja kwa moja.

4.6 Tunaweza pia kuhamishia Vigezo hivi vya Showmax kwa Makampuni Washirika kufuatia mageuzi katika Showmax Group, ikiwa ni pamoja na mabadiliko katika umiliki au udhibiti wa mali, hisa au usimamizi wa Showmax, au wa Makampuni yetu Washirika; uchakataji wa data yako binafsi kwa kusudi hili unalingana na maslahi yetu ya kisheria.

5. LINDA USALAMA NA USIRI WA AKAUNTI YAKO YA SHOWMAX, MAELEZO YA MALIPO, NENOSIRI NA KITAMBULISHO CHA MTUMIAJI

5.1 Baada ya kukamilisha utaratibu wa kujisajili kwenye Tovuti ya Showmax au kwenye Programu ya Showmax, tutakufungulia Akaunti ya Showmax. Utahitaji kutumia jina lako na jina la ukoo, anwani ya barua pepe, namba ya simu ya mkononi na nenosiri ili kuingia katika Akaunti yako ya Showmax na kutumia Huduma ya Showmax, au kitambulisho kingine kama hicho cha mtumiaji kama tunavyoweza kuruhusu mara kwa mara.

5.2 Unawajibika kwa matumizi yote ya Akaunti yako ya Showmax na nenosiri lako na kitambulisho chako kingine chochote cha mtumiaji (kwa mfano, maelezo ya kuingia katika akaunti za mitandao ya kijamii unazotumia kufikia Huduma ya Showmax, ikiwa inatumika).

5.3 Wakati wowote ambapo mtu anatumia Huduma ya Showmax, au kufanya kitendo kingine chochote kwa kutumia nenosiri lako kupitia Akaunti yako ya Showmax au kupitia matumizi ya kitambulisho chako cha mtumiaji, tutachukulia shughuli hii kana kwamba imefanywa nawe mwenyewe na kwa idhini yako.

5.4 Lazima uchukue hatua zote bora na zinazofaa za kutoruhusu kufikiwa, kuonyesha hadharani au kufanya nenosiri lako au kitambulisho chako cha mtumiaji au maelezo yako ya malipo au taarifa zako za malipo (kwa mfano, maelezo ya akaunti yako ya benki au kadi ya benki au njia nyingine ya malipo) yafikiwe na mtu yeyote ambaye hajaidhinishwa kuyafikia. Unakubali kuwa hatuwezi kukulinda usipofanya hivyo.

5.5 Lazima utufahamishe mara moja kwa kututumia barua pepe katika help@showmax.com ikiwa utashuku kuwa mtu mwingine amefikia Akaunti yako ya Showmax, au nenosiri au kitambulisho chako cha mtumiaji, au maelezo yako ya malipo au taarifa zako za malipo. Lazima pia utufahamishe mara moja kwa kututumia barua pepe katika help@showmax.com ikiwa utatambua kuwa Akaunti yako ya Showmax, au nenosiri au kitambulisho chako cha mtumiaji, au maelezo yako ya malipo yametumika bila idhini yako. Utawajibika kwa kubadilisha mipangilio yako ya faragha katika Akaunti yako ya Showmax, nenosiri, kitambulisho chako cha mtumiaji na maelezo yako ya malipo mara tu utakapotambua kuwa yamefikiwa au kutumika bila idhini yako.

5.6 Hatutawajibika kwa gharama au hasara yoyote utakayopata ikiwa mtu mwingine yeyote atatumia nenosiri, au kitambulisho chako cha mtumiaji, au maelezo yako ya malipo au taarifa za malipo kwa idhini au ruhusa yako.

6. VIFAA VYA KUFIKIA NA ZANA NA NYENZO ZINGINE

6.1 Una haki ya kutumia tu kisheria Huduma ya Showmax na kutiririsha au kupakua Maudhui kupitia njia zinazoruhusiwa na zilizobainishwa nasi, ambazo zinaweza kujumuisha kupitia Tovuti ya Showmax, au kwa kutumia Programu ya Showmax kwenye Kifaa cha Kufia kilichosajiliwa.

6.2 Tunaweza kuweka ukomo kwa idadi ya Vifaa vya Kufikia vilivyosajiliwa, na tunaweza kubadilisha kikomo hiki mara kwa mara.

6.3 Showmax inaweza kutoa mipango tofauti ya usajili kama sehemu ya Huduma ya Showmax. Kila aina ya mpango wa usajili itakuwa na vizuizi vya idadi ya mitiririsho sambamba ya Maudhui kwenye Kifaa cha Kufikia kilichosajiliwa katika Akaunti ya Showmax ya Mteja kwa mpango huo wa usajili. Baadhi ya mipango ya usajili inaweza kupatikana kwa Vifaa vya Kufikia vya mkononi pekee. Vizuizi hivi hubainishwa na Showmax, na unaweza kupata maelezo kutoka Showmax kabla ya kujisajili katika mpango wa usajili, yaani, wakati wa utaratibu wa kulipa. Idadi ya mitiririsho sambamba ya Maudhui inayoruhusiwa kwa Kifaa cha Kufikia kilichosajiliwa katika Akaunti yako ya Showmax wakati wowote itategemea aina mahususi ya Mpango wako wa Usajili. Hupaswi kupitisha idadi ya mitiririsho sambamba ya Maudhui kwa Kifaa cha Kufikia kilichosajiliwa katika Akaunti yako ya Showmax inayoruhusiwa katika Mpango wako mahususi wa Usajili.

6.4 Mipango ya Usajili ya Showmax:

6.4.1 Tunaruhusu ufikiaji wa Huduma ya Showmax kupitia Mipango mbalimbali ya Usajili kwa bei tofauti.

Unaweza kupata orodha ya Mipango yetu ya Usajili inayopatikana, bei yake na maelezo kuhusu maudhui yanayotolewa na Huduma ya Showmax katika https:/www.showmax.com.

6.5 Ili kufikia na kutumia Huduma ya Showmax, Vifaa vyako vya Kufikia lazima vitimize kikomo cha chini cha masharti ya kiufundi kama ilivyoelezwa kwenye Tovuti ya Showmax katika https://showmax.com/help/.

Hatutawajibika kwa njia yoyote kwa hali yako ya kushindwa kufikia Maudhui na Huduma ya Showmax kutokana na vizuizi vinavyohusiana na Vifaa vyako vya Kufikia.

6.6 Wewe unawajibika kwa gharama yako mwenyewe kununua na kulinda Vifaa vya Kufikia, huduma ya kutosha na ya kutegemewa ya intaneti na teknolojia yote ya mawasiliano na vifaa vya mawasiliano ya simu, zana, huduma, bidhaa, programu, mifumo, nyenzo na mengineyo, (“Teknolojia”) vinavyohitajika kufikia huduma ya intaneti au kutumia Huduma ya Showmax.

6.7 Ikiwa Kifaa cha Kufikia si chako, unathibitisha na kuahidi kuwa umepata ruhusa kutoka kwa mwenye Kifaa cha Kufikia ya kupakua au kutiririsha Maudhui kwenye Kifaa cha Kufikia kinachohusika na kutumia Kifaa cha Kufikia ili kupokea na kufikia Huduma ya Showmax.

6.8 Hatuwajibiki kwa gharama zozote za huduma ya intaneti, gharama za mtoa huduma na gharama za matumizi ya data. Lazima wewe au mwenye Kifaa cha Kufikia alipe gharama hizi.

6.9 Ubora wa Maudhui na Huduma ya Showmax, na uwezo wako wa kutumia Huduma ya Showmax na kutiririsha au kupakua Maudhui, ikiwa ni pamoja na muda unaochukuliwa kutiririsha au kupakua Maudhui na gharama husika, vinaweza kuathiriwa na sababu mbalimbali, kama vile mahali ulipo, kipimo cha data kinachopatikana, Vifaa vyako vya Kufikia na uwezo au utendakazi wake, kasi ya muunganisho wako wa intaneti, huduma zinazotolewa na watoa huduma wako na vifaa vya mawasiliano unavyotumia.

6.10 Hatutoi dhamana au mahakikisho yoyote kuhusu ubora wa hali yako ya utazamaji, au muda unaochukuliwa kutiririsha au kupakua Maudhui, au kipimo cha data au data nyingine itakayohitajika kutiririsha au kupakua Maudhui au kutumia Huduma ya Showmax.

6.11 Ikiwa wewe ni mteja wa Mipango yoyote ya Usajili ya Showmax iliyotajwa hapo juu, uwezo wako wa kutumia Mpango husika wa Usajili wa Showmax na kutiririsha na kupakua Maudhui, ikijumuisha muda unaochukuliwa kutiririsha Maudhui na gharama husika, vinaweza kuathiriwa na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na huduma zinazotolewa na Showmax. Hatuwajibiki kwa mapungufu yoyote ya ubora wa Maudhui yanayoweza kutokea au kutopatikana kwa Maudhui kuhusiana na Mpango wa Usajili wa Showmax.

7. MATUMIZI YANAYORUHUSIWA NA KILE AMBACHO HURUHUSIWI KUFANYA

7.1 Unapaswa tu kutumia Huduma ya Showmax kwa njia halali kwa njia ambayo tulikusudia hasa na kwa makusudi yako binafsi na yasiyo ya kibiashara (“Matumizi Yanayoruhusiwa”).

7.2 Hupaswi kufanya mambo yoyote yafuatayo moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja au kuruhusu mtu yeyote kuyafanya:

7.2.1 kufanya kitendo chochote kinachokiuka Vigezo hivi vyovyote vya Showmax au mwongozo au sera zetu zozote tulizochapisha;

7.2.2 kuonyesha, kusambaza, kuwasilisha, kutuma, kuchapisha au kutangaza Maudhui au Huduma ya Showmax kwa umma;

7.2.3 kufanya kitendo chochote ambacho ni kinyume cha sheria, cha udanganyifu au kinachokiuka au kuingia Haki zozote za Uvumbuzi zilizotajwa katika kifungu cha 16 hapa chini;

7.2.4 kutumia Teknolojia yoyote na yote au njia zingine za kufikia, kupanga, kuonyesha au kuunganisha kwenye Huduma ya Showmax (ikijumuisha Maudhui) kwa njia ambayo hatujaidhinisha moja kwa moja;

7.2.5 kutumia Teknolojia au njia zingine kuondoa, kuzima, kukwepa au kuzunguka ulinzi wowote wa Maudhui au mbinu za udhibiti wa ufikiaji, ikiwa ni pamoja na zile zilizokusudiwa kuzuia upakuaji, utiririshaji, unasaji, uunganisha, uonyeshaji, uzalishaji upya, ufikiaji, utumiaji au usambazaji wa Maudhui au Huduma ya Showmax;

7.2.6 kutumia Teknolojia au njia zingine kuondoa, kuzima, kukwepa au kuzunguka mbinu zozote za ulinzi wa Maudhui au Teknolojia nyingine au kutambua maelezo yaliyo kwenye Kifaa cha Kufikia;

7.2.7 kutumia Kifaa chochote cha Kufikia ambacho “kimedukuliwa” au “kuzibuliwa”;

7.2.8 kufikia Huduma ya Showmax (ikijumuisha Maudhui) kupitia njia zozote za kiotomatiki, ikiwa ni pamoja na kupitia matumizi ya “roboti,” “buibui,” au “visomaji vya nje ya mtandao” (mbali na utafutaji uliofanya mwenyewe kwenye mitambo ya kutafuta inayopatikana hadharani kwa kusudi pekee la, na kwa kiwango kinachohitajika tu kwa kubuni hifadhidata za tovuti na maudhui yake zinazopatikana hadharani - wala si akiba au kumbukumbu - ya Huduma ya Showmax au Maudhui na kutojumuisha hifadhidata au mitambo hiyo ya kutafuta inayopangisha, kutangaza au kuunganisha kimsingi kwa maudhui yanayokiuka au ambayo hayajaidhinishwa);

7.2.9 kuweka “virusi”, “trojan horses”, msimbo wa kompyuta, programu hasidi, maagizo, vifaa au vitu vingine vyovyote ambavyo vimebuniwa ili kukatiza, kuzima, kudhuru au vinginevyo kuzuia kwa namna yoyote utendaji wa Kifaa cha Kufikia, Teknolojia, huduma, data, kifaa cha kuhifadhi, programu, vifaa au mawasiliano yoyote, au vinginevyo kuathiri utendaji wake (“Msimbo Hasidi”) katika Maudhui au Teknolojia inayotumika na Showmax au mtu mwingine yeyote, ikijumuisha Tovuti ya Showmax, Programu ya Showmax au Huduma ya Showmax;

7.2.10 kuharibu, kuzima, kurundika, kuathiri au kuweza kufikia bila idhini Maudhui, Huduma ya Showmax, Tovuti ya Showmax, Teknolojia inayotumika na Showmax au watu wengine, au Akaunti za Showmax za Wateja au watumiaji wengine;

7.2.11 kuondoa, kubadilisha, kuzima, kuzuia, kuficha au vinginevyo kuathiri matangazo yoyote yanayoonyeshwa, au kutumika pamoja na Huduma ya Showmax (ikijumuisha Maudhui), Tovuti ya Showmax au Programu ya Showmax;

7.2.12 kutumia Huduma ya Showmax kutangaza bidhaa au huduma ambazo hatujaziidhinishwa moja kwa moja mapema kwa maandishi;

7.2.13 kukusanya au kuchakata maelezo kwa kukiuka Sera yetu ya Faragha;

7.2.14 kuhimiza tabia ambazo zinaweza kusababisha kosa la uhalifu au kusababisha kuchukuliwa hatua ya kiraia;

7.2.15 kuingilia hali ya mtu mwingine yeyote ya utumiaji na ufurahiaji halali na ulioidhinishwa wa Huduma ya Showmax, Tovuti ya Showmax, au Programu ya Showmax;

7.2.16 kujaribu kugundua au kufanya utafiti wa kuhandisi wa msimbo wa chanzo na nyenzo zingine ambazo ni sehemu ya Teknolojia inayotumika kutoa Huduma ya Showmax, au Maudhui, au Tovuti ya Showmax, au Programu ya Showmax;

7.2.17 kutoza pesa au kupokea hongo au kitu kingine kwa kuruhusu mtu mwingine yeyote kutumia au kufikia Huduma ya Showmax, Programu ya Showmax, Maudhui au Akaunti yako ya Showmax; na

7.2.18 kufanya kosa lingine lolote la ukiukaji wa Vizuizi vya Leseni, kama ilivyoelezwa katika Makubaliano ya Leseni (vyote vya hapo juu vinaitwa “Vitendo Visivyoruhusiwa”).

7.3 Vigezo hivi vya Showmax na vizuizi vyovyote kuhusu utumiaji wa Huduma ya Showmax vitatumika pia katika sehemu yoyote ya Tovuti ya Showmax, Programu ya Showmax na Maudhui ambayo huhifadhiwa unapotumia Huduma ya Showmax, Tovuti ya Showmax au Programu ya Showmax.

7.4 Tunaweza kutumia Teknolojia na njia zingine kuchunguza ikiwa unatii Vigezo hivi vya Showmax.

8. VIZUIZI VYA MAUDHUI, MABADILIKO KATIKA MAUDHUI NA HUDUMA YA SHOWMAX

8.1 Ni jukumu lako kuridhika na maudhui unayopendelea kutazama. Hakikisha kuwa kabla hujafikia Maudhui, Maudhui hayo yanatimiza masharti yako binafsi.

8.2 Isipokuwa iwe imeelezwa moja kwa moja katika Vigezo hivi vya Showmax, Maudhui haya hayakusudiwi, na hayapaswi kuchukuliwa kuwa ushauri au mapendekezo ya namna yoyote kabisa kuhusiana na, lakini si tu shirika, taasisi, uwekezaji, huduma au bidhaa yoyote.

8.3 Tunaweza kusasisha mara kwa mara Huduma ya Showmax, ikiwa ni pamoja na Maudhui. Tuna haki ya kufanya mabadiliko mara kwa mara katika jinsi tunavyotoa na kuendesha Huduma ya Showmax na Maudhui.

8.4 Tunaweza kwa hiari yetu:

8.4.1 kuchagua na kuamua Maudhui yatakayopatikana ili kutiririshwa au kupakuliwa, au kama sehemu ya Huduma ya Showmax;

8.4.2 kubadilisha, kuondoa au kusasisha mara kwa mara Maudhui yatakayopatikana ili kutiririshwa au kupakuliwa, au kama sehemu ya Huduma ya Showmax;

8.4.3 kuzuia Wateja au Watumiaji fulani Walioidhinishwa kufikia Maudhui au kuamua iwapo Maudhui fulani yatapatikana kwa Mteja au Mtumiaji yeyote Aliyeidhinishwa wakati wowote;

8.4.4 kudhibiti idadi ya vipindi au upakuaji wako wowote wa muda wa sehemu yoyote ya Maudhui au kupitia Akaunti ya Showmax wakati wowote;

8.4.5 kudhibiti idadi ya upakuaji wa muda wa kipindi fulani au sehemu ya Maudhui unaoweza kufanya au kuanzisha, au unaoweza kufanywa au kuanzishwa kupitia Akaunti ya Showmax;

8.4.6 kudhibiti idadi ya kiwango ambacho unaweza kujaribu kupakua kipindi fulani au sehemu ya Maudhui, ambapo upakuaji wa kipindi au sehemu ya Maudhui utashindwa kukamilika kwa sababu ya muunganisho dhaifu wa intaneti au tatizo lingine la kiufundi;

8.4.7 kufanya Maudhui tofauti yapatikane kwa Wateja au Watumiaji tofauti Walioidhinishwa katika maeneo tofauti;

8.4.8 kutumia Teknolojia na mbinu na kuchukua hatua za kuondoa na kufuta Maudhui na Maudhui yaliyopakuliwa kwenye Vifaa vya Kufikia na kufanya Maudhui na vipakuliwa hivyo visiweze kutazamwa; na

8.4.9 kutumia Teknolojia na mbinu za kusimba kwa njia fiche na kusimbua Maudhui na kulinda Maudhui yasitumike bila idhini na kudhibiti ufikiaji wa Maudhui.

8.5 Maudhui yanayoweza kupatikana ili kutazamwa yatatofautiana katika maeneo tofauti na tuna haki ya kuzuia Maudhui fulani yasitazamwe katika maeneo fulani.

8.6 Hupaswi kujaribu kufikia Maudhui yaliyozuiwa.

8.7 Tuna haki ya kutumia Teknoloji, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya kuzuia maudhui yasifikiwe katika eneo fulani. Hii inajumuisha Teknolojia yoyote ambayo inaweza kudhibiti au kuzuia ufikiaji wowote na/au kuzuia Maudhui, bidhaa au huduma yoyote isitumike na mtu kulingana na mahali ambapo mtu huyo alipo, na mbinu zingine ili kuthibitisha mahali ulipo na kuchunguza ili kubaini kuwa hufikii Maudhui yaliyozuiwa kutoka katika maeneo yaliyozuiwa.

9. UUNDAJI WA WASIFU, UDHIBITI WA WAZAZI NA USIMAMIZI WA WATUMIAJI WALIOIDHINISHWA

9.1 Kila Mteja anaweza kuunda idadi ya wasifu sita (6) katika Akaunti yake ya Showmax. Mteja anaweza kuunda wasifu wa watoto au wasifu wa kawaida, kuweka Mipaka ya Umri katika mipangilio ya kila wasifu (“Mipaka ya Umri”), na kudhibiti haki za Watumiaji Walioidhinishwa za kufikia wasifu mahususi. Kwa wasifu wa watoto, Mteja anaweza kuweka moja ya Mipaka ya Umri ifuatayo: Watoto Wadogo (A), Watoto Wakubwa (7-9 PG) au Vijana Wadogo (10-12 PG). Kwa wasifu wa kawaida, Mteja anaweza kuweka moja ya Mipaka ya Umri ifuatayo: Familia (PG), Vijana (13+ na 16+) au Watu Wazima (18+). Mteja anatakiwa kuthibitisha nenosiri lake ili kuweka au kurekebisha Mipaka ya Umri ya kila wasifu. Wasifu mkuu hauwezi kuwa wasifu wa watoto.

9.2 Mipaka ya Umri ikiwekwa katika wasifu, uchezaji wa video za Maudhui ambayo yamekadiriwa kuwa juu ya Mipaka ya Umri iliyowekwa katika wasifu huzuiwa. Ili kuzuia mtoto kubadili kwenda kwenye wasifu wenye Mipaka ya Umri wa juu ili kukwepa kizuizi cha kucheza video, Mteja anaweza pia kuweka PIN ya namba 4 kwa kila wasifu (“PINya Wasifu”). Katika hali hiyo, PIN ya Wasifu itahitajika wakati wowote ambapo Mtumiaji Aliyeidhinisha atajaribu kubadili wasifu au kuingia katika wasifu unaoilindwa na PIN ya Wasifu. Kuweka na/au kubadilisha PIN ya Wasifu pia kunahitaji nenosiri la Mteja.

9.3 Maudhui fulani yanaweza kuwa na Mipaka ya Umri, kuwa na lugha nzito, kuwa na picha zisizofaa au maudhui mengine yanayoweza kuwachukiza watazamaji wazingatifu au yasiyofaa kwa watazamaji wenye umri mdogo au aina fulani za watazamaji. Tutajaribu kutoa mwongozo wa hadhira unaofaa kuhusu Maudhui. Hata hivyo, ni jukumu la Mteja kutii maonyo hayo, kutenda kwa uwajibikaji na kuhakikisha kuwa hakuna watoto wadogo wanaoweza kufikia Maudhui ambayo hayawafai, hata kama PIN ya Wasifu imewekwa.

9.4 Mteja lazima asimamie hali zote za utumiaji wa Huduma ya Showmax kupitia Akaunti yake ya Showmax, na kila mtu anayetumia Vifaa vya Kufikia vilivyosajiliwa katika Akaunti ya Showmax Mteja lazima pia ahakikishe kuwa watu wote wanaotumia Huduma ya Showmax kupitia Akaunti yake, na kila mtu anayetumia Vifaa vya Kufikia vilivyosajiliwa katika Akaunti ya Showmax, anatii Vigezo hivi vya Showmax na hajihusishi katika Vitendo vyovyote Visivyoruhusiwa.

10. KIPINDI CHA USAJILI

10.1 Usajili wa Huduma ya Showmax utaanza wakati ambapo Mteja anajisajili ili kutumia Huduma ya Showmax na kununua angalau Mpango mmoja wa Usajili (ikijumuisha Jaribio la Bila Malipo, ikiwa linapatikana) na tumekubali usajili wake. Kipindi cha usajili cha kila Mpango wa Usajili ni labda mwezi mmoja au idadi nyingine ya siku tunazoweza kuidhinisha kuanzia siku ya kununua Mpango wa Usajili (“Kipindi cha Usajili”) Hata hivyo, ikiwa Mteja alipewa Jaribio la Bila Malipo, Kipindi cha Usajili kitahesabiwa kuanzia siku ya baada ya kuisha kwa Jaribio la Bila Malipo na kuendelea hadi siku inayolingana katika mwezi unaofuata (bila kujali kuwa kipindi cha usajili wako kilianza mwanzo wa kipindi cha Jaribio la Bila Malipo). Vilevile, Kipindi chochote cha Usajili ambacho si mwezi kilichotengewa Mpango wa Usajili kitaanza siku ya kununuliwa kwa Mpango huo wa Usajili na kuisha siku ya mwisho ya Kipindi cha Usajili.

10.2 Mteja anaweza kuchagua kati ya Mipango ya Usajili yenye malipo ya kujirudia (k.m, kila mwezi) au malipo ya mara moja.

10.3 Ikiwa Mteja atachagua Mpango wa Usajili wenye malipo ya kujirudia, Kipindi cha Usajili kitasasishwa kiotomatiki Tarehe ya Kulipa, kama inavyoelezwa hapa chini.

10.4 Ikiwa Mteja atachagua Mpango wa Usajili wenye malipo ya mara moja, usajili utakamilika baada ya kuisha kwa Kipindi cha Usajili kuanzia tarehe ambapo usajili ulinunuliwa, kulingana na Mpango wa Usajili uliochaguliwa. Unaweza kununua usajili mpya baada ya kukamilika kwa usajili wako wa malipo ya mara moja. Unaweza kununua usajili mpya baada ya kukamilika kwa usajili wako wa malipo ya mara moja.

10.5 Vigezo na masharti ya Jaribio la Bila Malipo

10.5.1 Mara kwa mara tunaweza kumruhusu Mteja kutumia Huduma ya Showmax ndani ya kipindi cha siku 14 baada ya Mteja kujisajili (au kipindi kingine tunachoweza kukibainisha baada ya kujisajili) na hatutamtoza Mteja kwa kutumia Huduma ya Showmax katika kipindi hiki; hii inajumuisha Mipango ya Usajili inayotolewa kupitia Vocha za Showmax na Showmax au kwa ushirikiano na washirika wengine kama ofa (“Jaribio la Bila Malipo”). Jaribio la Bila Malipo linahitaji Mteja achague njia ya malipo na kutoa maelezo ya malipo yanayohitajika. Tukimpa Mteja Jaribio la Bila Malipo na Mteja akose kulikatisha kabla ya mwisho wa kipindi cha Kujaribu Bila Malipo, Mteja atatakiwa kulipa Ada ya Usajili na usajili utaendelea kutumika na malipo ya kujirudia hadi sisi au Mteja atakapokomesha Makubaliano hayo kwa njia iliyoelezwa katika kifungu cha 14.

10.5.2 Isipokuwa kwa Mipango ya Usajili inayotolewa kama ofa, Majaribio ya Bila Malipo yanakusudiwa tu kutolewa kwa Wateja wapya. Hutatimiza sifa ya kupata Jaribio la Bila Malipo ikiwa maelezo yako ya malipo yametumika kwenye usajili katika Akaunti nyingine ya Showmax au ikiwa umewahi kujisajili.

10.5.3 We reserve the right, at our sole discretion, to determine whether you are entitled to a Free Trial. Ukikatisha usajili kabla ya kukamilika kwa Jaribio la Bila Malipo, hutaweza kufikia faili za muda ulizopakua baada ya kukamilika kwa Jaribio la Bila Malipo.

10.5.4 Ukikatisha usajili kabla ya kukamilika kwa Jaribio la Bila Malipo, utaendelea kufikia Huduma ya Showmax kwa kipindi kilichosalia cha Jaribio la Bila Malipo.

10.5.5 Tuna haki ya kuamua kwa hiari yetu mipango ya usajili ya Huduma ya Showmax inayoweza kuwa na Jaribio la Bila Malipo.

11. MALIPO NA UTOZAJI

11.1 Ada za usajili

11.1.1 Mteja lazima alipe Ada ya Usajili kila mwezi au kwa kipindi kingine tunachoweza kuweka mara kwa mara na ushuru wote tunaotakiwa kutoza kwenye ada hii (“Ada ya Usajili”) ili aweze kufikia Maudhui. Mteja hufahamishwa kuhusu jumla ya kiasi cha Ada ya Usajili wakati wa utaratibu wa kulipa kabla hajanunua Mpango wa Usajili.

11.1.2 Ada ya Usajili haijumuishi gharama zozote za intaneti, data, mtoa huduma au Kifaa cha Kufikia, ambazo unawajibika kulipia mwenyewe.

11.1.3 Mteja lazima alipe Ada ya Usajili mapema na kwa kila Kipindi cha Usajili.

11.1.4 Ukichagua Mpango wa Usajili wenye malipo ya kujirudia, usajili wako utasasishwa kiotomatiki baada ya kukamilika na tutakutoza kufikia au ndani ya kipindi kinachofaa baada ya siku inayolingana na siku ambayo ulinunua usajili wa kwanza (“Tarehe ya Kulipa”) Hata hivyo, ikiwa Mteja alipewa Jaribio la Bila Malipo, Tarehe ya Kulipa itahesabiwa kuanzia siku ya baada ya kukamilika kwa Jaribio la Bila Malipo (k.m., ikiwa Jaribio la Bila Malipo lilikamilika tarehe 15 Machi, Tarehe ya kwanza ya Kulipa itakuwa tarehe 16 Machi na siku ya 16 ya kila mwezi unaofuata).

11.1.5 Mteja lazima alipe Ada ya Usajili ifikapo kila Tarehe ya Kulipa. Ukichagua Mpango wa Usajili wenye malipo ya kujirudia, Ada ya Usajili itakatwa kiotomatiki kwenye akaunti yako kwa kutumia Njia ya Malipo unayochagua.

11.1.6 Ikiwa ungependa kubadilisha Mpango wako wa Usajili, lazima ukatishe Mpango wako wa sasa wa Usajili na ununue mpango mpya. Hata hivyo, una haki ya kununua Mpango wa Usajili wa ziada wa aina tofauti wakati wowote.

11.1.7 Showmax inaweza kutoza ada ndogo ya mara moja katika sarafu ya mahali ulipo ili kuthibitisha njia yako ya malipo. Utarejeshewa kiasi kitakachotozwa. Tafadhali kumbuka kuwa inaweza kuchukua siku kadhaa kwa pesa hizo kurejeshwa.

11.2 Mabadiliko kwa Ada ya Usajili

11.2.1 Tunaweza kurekebisha Ada zetu za Usajili mara kwa mara katika kipindi cha mkataba wetu nawe.

11.2.2 Tutampa Mteja taarifa ya mapema ya angalau siku 14 kuhusu marekebisho yoyote kwa Ada ya Usajili, isipokuwa tuwe hatuwezi kufanya hivyo kutokana na masharti ya sheria inayotumika (k.m., mabadiliko katika kiasi cha ushuru unaohusika).

11.2.3 Iwapo kutakuwa na marekebisho katika Ada ya Usajili na Mteja hakubali Ada ya Usajili iliyorekebishwa, Mteja anaweza kukatisha usajili wake kulingana na kifungu cha 14.1.

11.3 Njia ya Malipo

11.3.1 Ili kukamilisha utaratibu wa kujisajili, utatakiwa kutuambia njia utakayotumia kulipa (k.m, kwa kutumia kadi ya mikopo, kadi ya benki, kwa kutumia vocha, kupitia mshirika (ongeza kwenye bili) au njia nyingine ya malipo iliyowekwa katika Tovuti ya Showmax au Programu ya Showmax), (“Njia yako ya Malipo”) na kutupatia maelezo ya Njia yako ya Malipo yanayohitajika ili kulipa, (“Maelezo yako ya Malipo”).

11.3.2 Ukijisajili katika Huduma ya Showmax na kuweka Njia yako ya Malipo au Maelezo ya Malipo, unatupatia idhini ya kukutoza Ada ya Usajili kwa kiasi kinachotumika, na gharama zingine zozote unazoweza kutozwa kupitia utumiaji wa Huduma ya Showmax kupitia Maelezo na Njia yako ya Malipo.

11.3.3 Lazima utoe Maelezo ya Malipo ambayo ni sahihi, yanayotumika na yanayokubalika baada ya kujisajili, ambayo tunaweza kuyathibitisha. Maelezo hayo yatatumika kulipia Huduma ya Showmax kulingana na Njia ya Malipo uliyochagua na Mpango wa Usajili.

11.3.4 Ukiamua kuongeza Mpango mwingine wa Usajili, kulingana na kifungu cha 11.1.6, lazima utumie Njia moja ya Malipo uliyochagua kutumia katika Mpango wa Usajili unaotumika.

11.3.5 Ikiwa kutakuwa na mabadiliko katika Maelezo yako ya Malipo au Njia ya Malipo, unatakiwa kusasisha mara moja maelezo hayo kwa kuingia katika Tovuti ya Showmax au Programu ya Showmax na kusasisha Akaunti yako ya Showmax.

11.3.6 Lazima uhakikishe kila wakati kuwa unasasisha Maelezo yako ya Malipo na kuwa una pesa za kutosha kulipia Huduma ya Showmax.

11.3.7 Ukibadilisha Maelezo yako ya Malipo au Njia ya Malipo, tunaweza kuchagua kuthibitisha Maelezo hayo mapya ya Malipo au Njia ya Malipo kabla hatujakubali Maelezo hayo mapya ya Malipo au Njia ya Malipo. Tutakufahamisha mara tu tutakapokubali Maelezo yako mapya ya Malipo au Njia ya Malipo.

11.3.8 Ikiwa ulinunua Mpango wa Usajili wenye malipo ya kujirudia, unaweza kufuta Njia yako ya Malipo inayotumika, hata hivyo, unatakiwa kuibadilisha na Njia mpya ya Malipo na kutoa Maelezo ya Malipo yanayohitajika. Ikiwa hutaki kutoa Njia mpya ya Malipo, lazima ukatishe Usajili wako kulingana na kifungu cha 14.1 cha Vigezo hivi vya Showmax.

11.3.9 Tuna haki ya kukutoza Ada ya Usajili katika sarafu ya nchi yako au katika sarafu iliyoonyeshwa kwenye Tovuti ya Showmax wakati wa kulipa, kulingana na sheria zinazotumika.

11.3.10 Ikiwa malipo hayatakamilika au kupokewa, kwa sababu ya muda kuisha, ukosefu wa pesa za kutosha, Maelezo ya Malipo yasiyo sahihi au kwa sababu nyingine, unawajibika kwa malipo yoyote ambayo hayajapokewa na unatupatia idhini ya kuendelea kuchukua malipo kutoka kwenye Maelezo yako ya Malipo na Njia ya Malipo kwa kipindi cha siku za ziada kuanzia tarehe ambayo malipo yanafaa kulipwa.

11.3.11 Hatuwajibiki kwa vitendo, hitilafu, kucheleweshwa au usahaulifu kwa upande wa mshirika mwingine yeyote, benki, wakusanyaji wa malipo au watoa huduma za malipo. Utawajibika kwa vitendo, hitilafu, kucheleweshwa au usahaulifu kwa upande wa mshirika mwingine yeyote, benki, wakusanyaji wa malipo au watoa huduma za malipo, ikijumuisha wanaowajibika kwa Njia yako ya Malipo au kwa kutulipa.

11.3.12 Tutakufahamisha ikiwa malipo hayajakamilika na ikiwa hatuwezi kuchukua malipo kutoka kwenye Maelezo yako ya Malipo au kwa kutumia Njia yako ya Malipo. Tunaweza kusimamisha usajili wako wa Huduma ya Showmax ikiwa hatuwezi kuchukua malipo, kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 13.

11.3.13 Hata tukisimamisha usajili wako, bado utawajibika kwa malipo ambayo hayajapokewa ambayo unapaswa kutulipa kwa wakati ambao uliendelea kuwa mteja katika Huduma ya Showmax.

11.4 Bili na rekodi za mauzo

Tutampa Mteja rekodi ya mauzo ya malipo na historia ya oda ambayo Mteja anaweza kuiangalia kwa kuingia katika Akaunti ya Showmax ya Mteja kwenye Tovuti ya Showmax. Tunaweza pia kukutumia bili kupitia barua pepe.

11.5 Vocha na ofa za Showmax

11.5.1 Kwa makusudi ya sehemu hii, vocha inarejelea msimbo wa namba na herufi wa kutumika mara moja unaotolewa na Showmax au mshirika mwingine ambao Mteja lazima auwezeshe kwenye Tovuti ya Showmax, na ambao utakuwa na muda mfupi wa kutumika unaolingana na Kipindi cha Usajili cha Mpango wa Usajili uliochaguliwa.

11.5.2 Tunaweza kwa hiari yetu kutoa vocha sisi wenyewe au kupitia mipango yetu ya biashara na washirika wengine, kwa Wateja maalum, ambazo zinawawezesha Wateja kupata Huduma ya Showmax kwa bei iliyopunguzwa ya Ada ya Usajili au bila malipo, kulingana na vigezo na masharti yetu na ya washirika wetu. Iwapo hili litakuhusu, tafadhali kumbuka vigezo na masharti haya ya ziada. Vigezo na masharti yanayohusiana na vocha hizo na Showmax yatachapishwa kwenye Tovuti ya Showmax au katika njia zingine za mawasiliano zinazopatikana.

11.5.3 Iwapo utajisajili katika Mpango wa Usajili unaojirudia kwa kutumia vocha wakati wowote na iwapo muda wake wa kutumika utaisha, utatozwa kulingana na vigezo na masharti haya kwa kutumia Maelezo ya Malipo uliyotupatia.

11.5.4 Vocha zinazotolewa bila kulipishwa zinasimamiwa na Vigezo hivi vya Showmax yanayosimamia matumizi ya Majaribio ya Bila Malipo, hasa kifungu cha 10.5, isipokuwa ibainishwe wazi vinginevyo.

11.5.5 Vocha zinatumika tu kwa kipindi cha usajili kilichobainishwa katika Mpango wa Usajili katika tarehe ya kununuliwa. Tafadhali fahamu kuwa hatuongezi muda wa kutumika kwa vocha.

11.5.6 Tunaweza pia kuanzisha chaguo au Mipango kadhaa ya Usajili, ikijumuisha mipango maalum ya ofa yenye masharti na vizuizi tofauti. Vigezo vyovyote muhimu tofauti na vilivyoelezwa katika Vigezo hivi vya Showmax vitachapishwa kwenye Tovuti ya Showmax au katika njia zingine za mawasiliano zinazopatikana.

11.6 Marejesho ya Pesa

11.6.1 Kadri inavyoruhusiwa na sheria, malipo ya Ada ya Usajili hayawezi kurejeshwa na hatutarejesha au kukurejeshea salio kwa Vipindi vya Usajili ambavyo havijakamilika.

11.6.2 Iwapo ungependa kukomesha usajili wako, lazima ufanye hivyo kwa njia iliyoelezwa katika kifungu cha 14.1.

12. KUSIMAMISHWA KWA HUDUMA YA SHOWMAX AU MATUMIZI YAKO YA HUDUMA YA SHOWMAX

12.1 Tunaweza kusimamishwa kwa muda sehemu au Huduma yote ya Showmax, kutumika kwa Tovuti ya Showmax au Programu ya Showmax, au matumizi yako ya Huduma ya Showmax au Akaunti yako ya Showmax, katika hali moja au zaidi zifuatazo:

12.1.1 Tunahitaji kufanya matengenezo au kusasisha Tovuti ya Showmax, Programu ya Showmax au Teknolojia yoyote tunayotumia kutoa Huduma ya Showmax;

12.1.2 tutafahamu kuhusu tukio lolote halisi, linaloshukiwa au linaloweza kutokea la ulaghai au tukio halisi, linaloshukiwa au linaloweza kutokea la matumizi ambayo hayajaidhinishwa ya Tovuti ya Showmax, Programu ya Showmax, Huduma ya Showmax, Maudhui au Akaunti yako ya Showmax;

12.1.3 tuna sababu za kutosha kuamini kuwa Tovuti ya Showmax, Programu ya Showmax, Huduma ya Showmax au Maudhui yanatumika kiholela, kwa udanganyifu, kiharamu au kwa njia ambayo hatujaruhusu;

12.1.4 hutii wajibu wako na hata baada ya kukupa notisi ya siku 5 kutii (au kipindi kifupi kuliko hicho ambapo inafaa);

12.1.5 tuna sababu za kutosha kuamini kuwa nenosiri lako limepotea au limeibwa au limefichuliwe kwa mtu ambaye hajaidhinishwa;

12.1.6 tutafahamu kuwa maelezo yoyote uliyotoa ni ya uongo, si sahihi, hayajakamilika au yanapotosha;

12.1.7 ni lazima tufanye hivyo ili kutii sheria; au

12.1.8 tumeamrishwa kufanya hivyo na mahakama au msimamizi.

12.2 Tutaendelea kusimamisha huduma kwa muda ambao tunaamini kuwa unafaa.

12.3 Tutakufahamisha ikiwa tutasimamisha sehemu au Huduma yote ya Showmax au utumiaji wako wa Huduma ya Showmax au Akaunti yako ya Showmax, ambapo kuna sababu za kutosha kufanya hivyo.

13. KUSIMAMISHWA KWA HUDUMA YA SHOWMAX IWAPO HAIJALIPIWA

13.1 Tunaweza kusimamisha kwa muda sehemu au Huduma yote ya Showmax, au utumiaji wako wa Huduma ya Showmax au Akaunti yako ya Showmax ikiwa utashindwa kulipa kwa wakati au ikiwa tutashindwa kuchukua malipo kutoka kwenye Maelezo yako ya Malipo au kupitia Njia yako ya Malipo.

13.2 Tutakufahamisha kuwa tunasimamisha sehemu au Huduma yote ya Showmax, au utumiaji wako wa Huduma ya Showmax au Akaunti yako ya Showmax kwa sababu ya kutolipia.

13.3 Huduma itaendelea kusimamishwa hadi utakapolipa kiasi chote cha pesa tunachokudai.

13.4 Baada ya kulipa kiasi chote cha pesa tunachokudai, unaweza kuchagua iwapo:

13.4.1 ungependa kukomesha usajili wako katika Huduma ya Showmax kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 14.1; au

13.4.2 ungependa kuendelea kutumia usajili wako katika Huduma ya Showmax na Akaunti ya Showmax ambayo ilikuwa imesimamishwa.

14. KUKOMESHA MKATABA HUU

14.1 Jinsi ambavyo unaweza kukomesha Mkataba huu, ikiwa wewe ni Mteja

14.1.1 Unaweza kukomesha Mkataba huu na kukatisha usajili wako katika Huduma ya Showmax wakati wowote bila kutoa sababu.

14.1.2 Ili ukomeshe Huduma ya Showmax, lazima uingie katika Akaunti yako ya Showmax kwenye Tovuti ya Showmax na ufuate maagizo ya ukomeshaji.

14.1.3 Lazima ukatishe usajili wako kabla ya Tarehe ya Kutozwa inayofuata ili usitozwe malipo yanayofuata. Usipofanya hivyo, lazima ulipe Ada zote za Usajili ambazo tutakutoza kabla ya kukatisha usajili wako. Kadri inavyoruhusiwa na sheria, malipo yoyote ya Ada ya Usajili ambayo tayari yamelipwa katika tarehe ya kukatishwa hayatarejeshwa.

14.1.4 Ikiwa unatumia mshirika mwingine kama Njia ya Malipo na ungependa kukatisha usajili wako katika Huduma ya Showmax wakati wowote, unathibitisha na kukubali kuwa huenda pia ukahitaji kukomesha uhusiano wako na mshirika huyo mwingine kwa kufunga akaunti yako uliyofungua na mshirika mwingine anayehusika. Maelezo ya malipo kuhusiana na usajili wako katika Huduma ya Showmax yanaweza kuwekwa wazi katika akaunti yako na mshirika mwingine anayehusika.

14.2 Ikiwa wewe ni Mtumiaji Aliyeidhinishwa, unaweza kukomesha Mkataba huu kati yako na Showmax kwa kuacha kutumia Huduma ya Showmax.

14.3 Jinsi tunavyoweza kukomesha Mkataba huu:

14.3.1 Tuna haki ya kukomesha Mkataba wetu nawe wakati wowote na kwa sababu yoyote, au usajili wako katika Huduma ya Showmax, au utumiaji au upatikanaji wa Huduma ya Showmax, au haki yako ya kutumia Huduma ya Showmax au sehemu yake yoyote. Tukifanya hivyo na wewe ni Mteja, tutakupa notisi ya mapema ya siku 30 (isipokuwa tuwe tunatakiwa kukomesha mkataba kisheria au inafaa kutoa notisi ya fupi kulingana na hali).

14.3.2 Tunaweza kukomesha Mkataba na kukomesha utumiaji wako wa Huduma ya Showmax, Maudhui na Tovuti ya Showmax mara moja wakati wowote katika hali moja au zaidi zifuatazo:

14.3.2.1 ukikiuka sharti muhimu la Vigezo hivi vya Showmax, na ukose kurekebisha kosa hilo baada ya kukupa notisi ya siku 5 (au kipindi kifupi ambapo inafaa);

14.3.2.2 ukikiuka Makubaliano ya Leseni;

14.3.2.3 tukiwa na sababu za kutosha kuamini kuwa unafanya au umefanya Kitendo Kisichoruhusiwa;

14.3.2.4 ukijaribu kufikia Maudhui yaliyozuiwa katika maeneo yaliyozuiwa;

14.3.2.5 tukiwa na sababu za kutosha kuamini kuwa unajihusisha katika matumizi haramu au yasiyo ya Huduma ya Showmax au Maudhui;

14.3.2.6 ikiwa ni lazima tufanye hivyo ili kutii sheria;

14.3.2.7 tukiambiwa na mahakama au msimamizi kuwa tufanye hivyo; au

14.3.2.8 ikiwa sharti lolote katika Vigezo hivi vya Showmax, au sehemu ya sharti haitaweza kutekelezwa, itakuwa kinyume cha sheria au itakuwa si sahihi.

15. ATHARI ZA KUKOMESHWA

15.1 Athari za iwapo utakomesha Mkataba huu

Ukikomesha Mkataba huu, utaendelea kuwa na haki za kutumia Huduma ya Showmax hadi mwisho wa Kipindi cha Usajili wako wa sasa na utaondolewa katika Huduma ya Showmax siku ya kabla ya Tarehe ya Malipo inayofuata. Huduma ya Showmax itaendelea kupatikana hadi siku ya kabla ya Tarehe ya Malipo inayofuata hata kama Akaunti yako ya Showmax haitumiki au hutumii Huduma ya Showmax kwa muda uliosalia wa Kipindi cha Usajili baada ya kukomesha huduma. Hii inamaanisha kuwa utaweza kupata Huduma ya Showmax na Maudhui kwa muda uliosalia wa kipindi hicho.

15.2 Athari za iwapo tutakomesha Mkataba huu

Tukikomesha Mkataba huu au haki zako za kutumia Huduma ya Showmax, haki zako za kutumia Maudhui na Huduma ya Showmax zitakoma tarehe ambayo tutakoma kukuruhusu kutumia Huduma ya Showmax. Lazima uacha kutumia Huduma ya Showmax na Maudhui kuanzia tarehe hiyo.

15.3 Vigezo ambavyo havikomi kutumika

15.3.1 Masharti haya ya Vigezo hivi vya Showmax yataendelea kutumika baada ya kukomeshwa kwa Mkataba huu au usajili wako katika Huduma ya Showmax, ikiwa ni pamoja na vigezo na masharti ambayo kwa jinsi yalivyo lazima yaendelee kutumika. Hii ni kwa sababu haki na wajibu fulani lazima viendelee kutumika hata kama Mkataba kati yetu umekomeshwa au umeacha kutumia Huduma ya Showmax.

15.3.2 Baadhi ya masharti katika Vigezo hivi vya Showmax ambayo yataendelea kutumika ni pamoja na (lakini si tu):

15.3.2.1 vigezo na masharti ambapo dhima au wajibu wetu, au wa Makampuni zetu Washirika, yametengwa au yamedhibitiwa, ikiwa ni pamoja na kiasi cha pesa ambacho unaweza kudai kutoka kwetu;

15.3.2.2 vigezo na masharti ambapo haki ulizo nazo dhidi yetu, au Makampuni zetu Washirika, yamedhibitiwa au yametengwa;

15.3.2.3 vigezo na masharti ambayo yanatulinda sisi au Makampuni zetu Washirika, au yanayokuwajibisha kwa hasara na uharibifu fulani unaoweza kutokea;

15.3.2.4 haki zetu katika kifungu cha 8.4;

15.3.2.5 masharti yaliyo katika kifungu cha 16; na

15.3.2.6 vigezo na masharti mengine yoyote yaliyo katika Vigezo vya Showmax ambavyo vimebainishwa wazi kuwa vitaendelea kutumika baada ya kukomeshwa kwa Mkataba huu, au baada ya kukomeshwa kwa sehemu yoyote ya Mkataba huu.

16. MALI YA UVUMBUZI

16.1 Unathibitisha kuwa Maudhui yanayotolewa kupitia Huduma ya Showmax yanamilikiwa na, au tumepewa leseni yake na yanalindwa na sheria, ikiwa ni pamoja na sheria ya mali ya uvumbuzi.

16.2 Hupaswi kutumia Huduma ya Showmax au Maudhui kwa njia yoyote ambayo ni kinyume cha sheria (ikiwa ni pamoja na sheria ya mali ya uvumbuzi), au inayoingilia au kutumia vibaya haki zetu (ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, Haki za Mali ya Uvumbuzi), au haki au Haki za Mali ya Uvumbuzi za Makampuni zetu Washirika, watoa leseni au mshirika mwingine yeyote. Katika Vigezo hivi vya Showmax, “Haki za Mali ya Uvumbuzi” inajumuisha haki za mali ya uvumbuzi za namna na hali yoyote, ikiwa ni pamoja na (lakini si tu) hakimiliki, hataza, haki za hataza, miundo, haki za miundo, haki za uvumbuzi, haki za hifadhidata, ujuzi, maelezo ya siri, siri za biashara, chapa za biashara, majina ya biashara, majina ya vikoa, alama za huduma, nia njema na haki nyingine zote za mali ya uvumbuzi, iwe zimesajiliwa au hazijasajiliwa, ambazo zitaendelea kutumika au zitaendelea kutumika kwa sasa au baadaye katika sehemu yoyote duniani, na ikiwa ni pamoja na haki zote za kudai fidia ya uharibifu wa mali kutokana na ukiukaji, uingiliaji au matumizi mabaya ya Haki hizo zozote za Mali ya Uvumbuzi.

16.3 Hupaswi kuiga, kubadilisha, kunakili, kutekeleza, kutuma au kutumia kibiashara Maudhui kwa namna yoyote ile, na hakuna Maudhui yanayotolewa kwa Kifaa cha Kufikia yanayopaswa kusambazwa upya au kunakiliwa kutoka kwenye Kifaa hicho cha Kufikia.

16.4 Haki zote za Mali ya Uvumbuzi, ikiwa ni pamoja na haki, sehemu na maslahi katika na kwenye Huduma ya Showmax, Tovuti ya Showmax, Programu ya Showmax na Maudhui, vya namna yoyote ile vilivyopo kwa sasa na vya baadaye, vinabaki kuwa mali yetu kamili na ya watoa leseni wetu.

16.5 Hupaswi wakati wowote kununua haki, sehemu, umiliki au maslahi, ikiwa ni pamoja na Haki za Mali ya Uvumbuzi, katika au kwenye Huduma ya Showmax, Tovuti ya Showmax, Programu ya Showmax au Maudhui kuliko leseni inayodhibitiwa, isiyo ya kipekee, isiyoweza kuhamishwa na inayoweza kubatilishwa ya kutumia Huduma ya Showmax kwa Matumizi Yanayoruhusiwa kulingana na Vigezo hivi vya Showmax.

16.6 Tukiwa tumepewa leseni ya Maudhui yoyote au ni ya mshirika mwingine yeyote, haki zako za kuyatumia zitasimamiwa pia na vigezo na masharti yoyote ambayo mtoa leseni au mshirika huyo mwingine ataweka mara kwa mara, na unakubali kutii vigezo na masharti hayo ya mshirika mwingine.

16.6 Kwa kuondoa shaka, hatua ya kuweka Mkataba au kutumia Huduma ya Showmax haikupi haki zozote kwenye au katika Haki za Mali ya Uvumbuzi za mshirika mwingine yeyote au mifumo ya mshirika mwingine, na teknolojia, programu, vijenzi, API, zana za programu au huduma au nyenzo zingine zilizo chini ya leseni au zinazotolewa na au kwa niaba ya mshirika mwingine yeyote.

17. KANUSHO NA KUONDOLEWA KWA DHAMANA

17.1 Kadri inavyoruhusiwa na sheria, Huduma ya Showmax, Programu ya Showmax na Maudhui vinatolewa kwa msingi wa "jinsi ilivyo" na bila mahakikisho au dhamana zozote, iwe za wazi, zinazodhaniwa au za kisheria (ikwia ni pamoja na dhamana zozote zinazodhaniwa za kutegemewa, ufaafu kwa kusudi fulani au kutokuwa na hitilafu au kasoro).

17.2 Kadri inavyoruhusiwa na sheria, hatutoi mahakikisho na hatutoi dhamana kuwa Huduma ya Showmax au Maudhui yataboreshwa ili kutimiza matarajio au mahitaji yako binafsi, itapatikana na kufikiwa kila wakati, haitakatizwa, haitakuwa na hitilafu, itakuwa salama au haitakuwa na Msimbo Hasidi.

18. VIKOMO VYA DHAMANA YETU

18.1 Kadri inavyoruhusiwa na sheria, sisi na Mshirika wetu hatutawajibika kwako (na tunakanusha dhima yote) kwa hasara, dhima, jeraha au uharibifu wowote wa mali (uwe wa moja kwa moja, usio wa moja kwa moja, maalum, wa adhabu au unaoambatana) wa namna yoyote kutokana na:

18.1.1 hitilafu, makosa au kasoro zozote katika Maudhui au Huduma ya Showmax;

18.1.2 jeraha binafsi au uharibifu wa mali wa namna yoyote ile, kutokana na ufikiaji na utumiaji wa Huduma ya Showmax;

18.1.3 ufikiaji au utumiaji wowote ambao haujaidhinishwa wa Teknolojia yetu na/au maelezo yote binafsi yaliyohifadhiwa humo;

18.1.4 hali yoyote ya kukatizwa au kuacha kutumwa kwa maudhui kwenye au kutoka katika Programu ya Showmax, Maudhui au Teknolojia tunayotumia kutoa au kupokea Huduma ya Showmax au Maudhui; na/au

18.1.5 Msimbo wowote Hasidi unaoweza kutumwa kwenye au kupitia Programu ya Showmax, Tovuti ya Showmax, Huduma ya Showmax au Maudhui.

18.2 Masharti ya kifungu cha 18.1 yanatumika bila kujali iwapo dai lolote ambalo wewe au wengine wanawasilisha, au hasara, dhima, jeraha au uharibifu wowote wa mali uliopata, unatokana na dhamana, mkataba, ukiukaji au nadharia nyingine yoyote ya kisheria, na iwapo tumefahamishwa au hatujafahamishwa kuhusu uwezekano wa kutokea kwa uharibifu huo wa mali.

18.3 Licha ya masharti ya hapo juu ya kifungu cha 18, madai yoyote yanayowasilishwa kuhusiana na Programu ya Showmax au Huduma ya Showmax yatawasilishwa dhidi ya Showmax wala si kwa mshirika mwingine yeyote, ikiwa ni pamoja watoa leseni au watoa huduma wetu. Kadri inavyoruhusiwa na sheria inayotumika, watoa leseni na watoa huduma wetu hatawajibika kwako kuhusiana na Programu ya Showmax au Huduma ya Showmax.

19. FIDIA

19.1 Kadri inavyoruhusiwa na sheria, unakubali wazi kutufidia sisi na Mshirika wetu na unakubali kutotuwajibisha sisi, Mshirika wetu na watoa huduma wetu dhidi ya hasara, dhima, gharama na uharibifu wowote wa mali ambao sisi au wao wanaweza kupata kutokana na:

19.1.1 wewe kuingilia au kutumia vibaya haki za mtu yeyote, ikijumuisha Haki za Mali ya Uvumbuzi kuhusiana na Huduma ya Showmax na Maudhui;

19.1.2 wewe kufanya Kitendo Kisichoruhusiwa;

19.1.3 wewe kutotii Vigezo hivi vya Showmax; na/au

19.1.4 kitendo chochote cha kimakusudi au cha kinyume cha sheria unachofanya au kutochukua hatua.

20. NOTISI NA MAWASILIANO

20.1 Notisi zozote tunazotumiwa chini ya Vigezo hivi vya Showmax, ikiwa ni pamoja na notisi za kisheria, lazima ziwasilishwe kwetu kupitia barua pepe katika help@showmax.com au kwa mkono au kwa njia ya posta kwa anwani ifuatayo:

20.1.1 ikiwa unapokea Huduma ya Showmax kutoka kampuni ya Showmax SA Proprietary Limited, iliyoko: 144 Bram Fischer Drive, Randburg, Johannesburg, Gauteng, 2194, Afrika Kusini;

20.1.2 ikiwa unapokea Huduma ya Showmax kutoka kampuni ya MSAT Nigeria Limited, iliyoko: Plot 1381 Tiamiyu Savage Street, Victoria Island, Lagos, Naijeria;

20.1.3 ikiwa unapokea Huduma ya Showmax kutoka kampuni ya Showmax Africa Holdings Limited, iliyoko: 27 Old Gloucester Street, London, Uingereza, WC1N 3AX, Uingereza.

20.2 Notisi zozote tunazokutumia chini ya Vigezo hivi ya Showmax, ikiwa ni pamoja na notisi za kisheria, zitawasilishwa kwako kwa kutumia Maelezo ya Mawasiliano au kupitia njia yoyote iliyotajwa katika kifungu cha 20.3 hapa chini, kwa hiari ya Showmax. Notisi zozote tunazoweza kukutumia na ambazo unapokea, itazingatiwa kuwa notisi ya kutosha.

20.3 Pia, tuna haki ya kukutumia notisi na mawasiliano kuhusu masuala fulani kupitia SMS, au barua pepe au unapoingia katika Akaunti ya Showmax, au kwenye Tovuti ya Showmax, au kupitia Programu ya Showmax. Masuala haya ni pamoja na:

20.3.1 kuongezwa kwa Ada za Usajili;

20.3.2 mabadiliko au marekebisho ya maelezo yako;

20.3.3 kusimamishwa kwa Akaunti yako ya Showmax;

20.3.4 notisi za kukufahamisha kuwa umekiuka Vigezo hivi vya Showmax;

20.3.5 notisi za kusimamishwa au kukomeshwa kwa, au kuwa tuna nia ya kusimamisha au kukomesha Mkataba huu au Huduma ya Showmax au utumiaji wako wa Huduma ya Showmax (au sehemu yake yoyote);

20.3.6 notisi za kukufahamisha kuwa tumebadilisha sehemu yoyote ya Vigezo vya Showmax; na

20.3.7 notisi kuhusu maelezo ya bili au malipo, ikiwa ni pamoja na (lakini si tu) kutolipa.

20.4 Hupaswi kujiondoa katika huduma ya kupokea notisi kulingana na kifungu cha 20.3 na mawasiliano kama hayo yanayohusiana na utumiaji wako wa Huduma ya Showmax na uhusiano wetu wa kimkataba.

20.5 Baada ya kujisajili, tunaweza kutumia Maelezo yako ya Mawasiliano kukupa habari zinazohusiana na Huduma ya Showmax, pamoja na taarifa na ofa mpya ambazo Showmax inatoa kama sehemu ya Huduma ya Showmax (“Mawasiliano ya Matangazo”). Njia zetu za Mawasiliano ya Matangazo zinaweza kujumuisha barua pepe, SMS, mifumo mingine ya mawasiliano (k.m., WhatsApp), kupiga simu au njia yoyote ya mawasiliano inayostahili ambayo Showmax inaweza kutumia mara kwa mara. Ukijisajili katika Showmax, unaipa Showmax ruhusa ya kukutumia Mawasiliano ya Matangazo kadri iliyoelezwa hapo juu. Unaweza kujiondoa (na kujijumuisha tena, ukipenda) katika huduma ya kupokea Mawasiliano ya Matangazo kutoka Showmax wakati wowote katika mipangilio ya Akaunti yako ya Showmax au kwa kutumia chaguo la kujiondoa lililojumuishwa katika mawasiliano hayo yoyote (k.m., kwa kutumia msimbo uliowekwa katika kila SMS au kwa kubadilisha mapendeleo yako ya matangazo katika mipangilio ya akaunti yako ya WhatsApp au mfumo mwingine wa mawasiliano). Ikiwa unahitaji usaidizi wa kubadilisha mapendeleo yako ya matangazo, unaweza kuomba usaidizi kwa kutumia njia zilizoelezwa katika kifungu cha 20.7 hapa chini.

20.6 Notisi zote tunazotoa kwa Mteja zitazingatiwa kuwa zimetolewa, na kuchukuliwa kuwa pia zimetolewa kwa Watumiaji Walioidhinishwa wanaofikia au kutumia Huduma ya Showmax kupitia Akaunti ya Showmax ya Mteja. Notisi zote tunazotoa kwa Mtumiaji Aliyeidhinishwa zitazingatiwa pia kuwa zimetolewa, na kuchukuliwa kuwa pia zimetolewa kwa Mteja ambaye Akaunti yake ya Showmax inatumiwa na Mtumiaji Aliyeidhinishwa. Mteja na Watumiaji Walioidhinishwa lazima wafahamishane mara moja kuhusu notisi wanazoweza kupokea kutoka kwetu.

20.7 Iwapo utakuwa na maswali yoyote kuhusiana na utumiaji wako wa Huduma ya Showmax, unaweza kufikia Kituo chetu cha Usaidizi katika https://showmax.com/help/ na kupata usaidizi kupitia gumzo la moja kwa moja, au ututumie barua pepe katika help@showmax.com. Unaweza pia kuwasiliana na huduma yetu ya usaidizi kwa nambari +255 (0)768 988800, +255(0)784104700, +255(0)222199600. Tafadhali kumbuka kuwa unaweza kutozwa ada kupiga simu.

21. MAREJELEO NA VIUNGO VYA, NA KUTOKA KWENYE TOVUTI, BIDHAA NA HUDUMA ZINGINE

21.1 Programu ya Showmax na Tovuti ya Showmax vinaweza kuwa na njia za kufikia bidhaa na huduma zinazotolewa na washirika wengine. Bidhaa na/au huduma hizo zinaweza kutolewa moja kwa moja au kupitia viungo vya washirika wengine. Panapofaa, tutabainisha bidhaa na/au huduma kama bidhaa au huduma za washirika wengine. Licha ya kwamba bidhaa na/au huduma zinaweza kutolewa kwa ushirikiano, unathibitisha kuwa mkataba wa utoaji wa bidhaa au huduma hiyo ya mshirika mwingine ni kati yako na mshirika huyo mwingine anayehusika na hatutahusika katika mkataba huo. Isitoshe, hatutawajibika kwa kitendo au usahaulifu wowote wa mshirika mwingine, wala utoaji wa bidhaa au huduma kwako kutoka kwa mshirika mwingine.

21.2 Programu ya Showmax na Tovuti ya Showmax vinaweza kuwa na marejeleo au viungo vya tovuti zingine (“Tovuti Zingine”) na bidhaa, maoni au huduma za washirika wengine. Marejeleo au viungo hivi havikusudiwi kuwa, na havipaswi kuchukuliwa kuwa uidhinishaji, upendekezaji au ushirikiano na Tovuti hizi Zingine au maoni, bidhaa au huduma za washirika wengine. Marejeleo au viungo hivi havikusudiwi kuwa, na havipaswi kuchukuliwa kuwa uidhinishaji, upendekezaji au ushirikiano na Tovuti hizi Zingine au maoni, bidhaa au huduma za washirika wengine. Utumiaji wako wa Tovuti Zingine au bidhaa au huduma za washirika wengine utakuwa kwa tahadhari yako binafsi.

21.3 Kadri inavyoruhusiwa na sheria, hatuwajibiki kwako kwa hasara, dhima, gharama, dai, faini au uharibifu wowote wa mali, uwe wa moja kwa moja, usio wa moja kwa moja, maalum au wa kuambatana, unaotokana na au unaohusiana na utegemeaji, utumiaji au jaribio la kutumia Tovuti Zingine au maoni, bidhaa au huduma za washirika wengine.

21.4 Hupaswi kamwe (na hupaswi kuruhusu mshirika mwingine yeyote) kuturejelea sisi, Huduma ya Showmax, Programu ya Showmax au Maudhui, iwe kupitia kwa kiungo au njia nyingine, ambapo marejeleo hayo yanaweza kufafanuliwa kwa njia yoyote kuwa ni uidhinishaji, ushirikiano au upendekezaji wetu kuhusiana nawe au mshirika mwingine, au wa huduma, bidhaa, maoni au mwenendo wako au wa mshirika mwingine.

22. MASHARTI YA ZIADA

22.1 Vigezo hivi vya Showmax au Makubaliano na haki, wajibu na leseni zozote zinazotolewa hapa, havipaswi kuhamishwa, kutolewa kwa mwingine, kukabidhiwa au kupeanwa nawe.

22.2 Unakubali kuwa wakati wowote, tunaweza kuhamisha, kutoa kwa mwingine, kukabidhi au kupeana haki na wajibu wetu wowote au wote chini ya Makubaliano au Vigezo hivi vya Showmax na tunaweza kufanya hivyo bila idhini yako. Tutakufahamisha iwapo tutahamisha, tutatoa kwa mwingine, tutakabidhi au tutapeana haki au wajibu wowote kwa mshirika mwingine, isipokuwa kwamba si lazima tukufahamishe iwapo tutahamisha, tutatoa kwa mwingine, tutakabidhi au kupeana haki au wajibu wowote au wote kwa Mshirika wetu. Tunaweza kukabidhi wajibu wetu kwa washirika wengine bila idhini yako, na si lazima tukufahamishe iwapo tutakabidhi wajibu wetu wowote kwa washirika wengine.

22.3 Vigezo hivi vya Showmax vitatumika kwa faida ya, na kufuatwa na warithi na wawakilishi wa kila mshirika.

22.4 Tusipotekeleza au kutumia haki au sharti lolote la Vigezo hivi vya Showmax hakitakuwa kitendo cha uachiliaji wa haki au sharti hilo.

22.5 Vigezo hivi vya Showmax, ikiwa ni pamoja na hati zilizorejelewa hapa, vinaunda makubaliano yote kati yako nasi kuhusiana na utumiaji wa Maudhui na Huduma ya Showmax. Kadri inavyoruhusiwa na sheria, wewe au sisi hatuna wajibu wa kisheria wa kutii sheria, sharti, dhamana, hakikisho au ahadi yoyote kuhusiana na Huduma ya Showmax au Maudhui, ambayo haijaandikwa katika Vigezo hivi vya Showmax.

22.6 Kila sharti la Vigezo hivi vya Showmax, na kila sehemu ya sharti lolote, inaweza kuondolewa na kutengwa na masharti mengine. Kadri inavyoruhusiwa na sheria, iwapo sharti lolote la Vigezo hivi vya Showmax, au sehemu ya sharti haitaweza kutekelezwa, itakuwa kinyume cha sheria au si sahihi, lazima ichukuliwe kana kwamba haikujumuishwa katika Vigezo hivi vya Showmax, Vigezo hivi vya Showmax vilivyobaki bado vitatumika na kutekelezwa.

22.7 Vigezo hivi vya Showmax vinaweza kutolewa katika lugha kadhaa. Iwapo kutakuwa na tofauti yoyote, Toleo la Kiingereza litatumika.

22.8 Katika Vigezo hivi vya Showmax, vichwa vimewekwa ili kurahisisha mambo wala si kutumika katika kufafanua vigezo hivi, na isipokuwa ielezwe wazi vinginevyo au vinginevyo ihitajike kulingana na muktadha:

22.8.1 marejeleo ya umoja yanajumuisha wingi na kinyume chake;

22.8.2 maneno yaliyo katika jinsia fulani yanajumuisha jinsia zingine (mwanamume, mwanamke na jinsi isiyoegemea upande wowote). Marejeleo ya jinsia isiyoegemea upande wowote (kwa mfano 'wao' au 'hicho') inajumuisha jinsia zote;

22.8.3 maneno au vifungu ambavyo vimefafanuliwa au kuandikwa kwa herufi kubwa katika Vigezo hivi vya Showmax, vitakuwa na maana sawa vinapotumika katika Vigezo hivi vya Showmax;

22.8.4 neno ‘ikiwa ni pamoja na’ au 'inajumuisha' au ' pamoja na' halipaswi kuchukuliwa kuwa linatumika tu kwa orodha inayofuata neno hilo au haijumuishi vitu vingine kwenye orodha inayofuata neno hilo. Neno:

22.8.4.1 'ikiwa ni pamoja na' inamaanisha 'ikiwa ni pamoja na, lakini si tu';

22.8.4.2 'inajumuisha' inamaanisha 'ni pamoja na, lakini si tu'; na

22.8.4.3 'pamoja na' inamaanisha 'pamoja na, lakini si tu'; na

22.8.5 iwapo idadi yoyote ya siku imetolewa, siku hizo zinahesabiwa bila kujumuisha siku ya kwanza lakini zinajumuisha siku ya mwisho.