Vigezo Vya Utumiaji Wa Tovuti Ya Showmax

1. Utangulizi

1.1 Showmax ("Showmax" au "sisi" au "nasi" au "yetu") inatoa huduma ya utazamaji wa maudhui popote ulipo ("Huduma ya Showmax") ambayo watumiaji wanaweza kuitumia kutazama au kupakua kwa muda vipindi vya televisheni, filamu, video au klipu za sauti na maudhui mengine kama hayo ya sauti na picha (“Maudhui") kwa kutumia kifaa cha kielektroniki kinachoweza kuunganishwa kwenye intaneti, ikijumuisha kompyuta za watu binafsi, simu za mkononi, vishikwambi, vicheza faili za sauti na video, televisheni janja (Smart TV), ving'amuzi, vifaa vya michezo ya video na vifaa vingine kama hivyo ("Kifaa cha Kufikia").

1.2 Hivi ni vigezo na masharti ya jumla, yanayoweza kurekebishwa mara kwa mara ("Vigezo vya Utumiaji") vinavyotumika wakati mtu ("Mtumiaji" au "yako" au "wewe") anafikia na kutumia tovuti inayopatikana katikat https://showmax.com na URL nyingine yoyote tunayotumia mara kwa mara ("Tovuti ya Showmax").

1.3 Ukitumia Tovuti ya Showmax, unakubali kuwa umesoma, umeleewa na unakubali kufuata Vigezo vya Utumiaji vilivyochapishwa kwenye Tovuti ya Showmax wakati unapoifikia na kuitumia.

1.4 Vigezo na masharti ya ziada yanaweza kutumika kwa maelezo, maudhui, huduma, programu au kipengele kingine chochote cha Tovuti ya Showmax au kwa bidhaa na/au huduma tunazotoa ("Vigezo vya Ziada"). Iwapo kutakuwa na tofauti kati ya Vigezo hivi vya Utumiaji na Vigezo vya Ziada, Vigezo hivi vya Utumiaji vitatumika

1.5 Tafadhali kumbuka kuwa sera yetu ya faragha, inayopatikana katika https://showmax.com/privacy/ ("Sera ya Faragha") imejumuishwa katika Vigezo hivi vya Utumiaji.

2. Maunzi, programu na ufikiaji wa intaneti

2.1 Ni wajibu wako kununua na kutunza kompyuta na programu, vifaa vya mawasiliano ya simu na huduma za ufikiaji wa intaneti kwa gharama yako ("Vifaa vya Teknolojia ya Mawasiliano") ili kufikia na kutumia Tovuti ya Showmax.

2.2 Lazima uhakikishe, kabla hujaanza kutumia Tovuti ya Showmax wakati wowote, kuwa Tovuti ya Showmax inatumika katika Vifaa vyako vya Teknolojia ya Mawasiliano na kuwa Vifaa vyako vya Teknolojia ya Mawasiliano vinafaa ili uweze kufikia na kutumia Tovuti ya Showmax.

2.3 Unakubali kuwa hutatumia au kujaribu kutumia Tovuti ya Showmax kwa njia yoyote isipokuwa kupitia mfumo tunaotoa.

2.4 Hatutawajibika kwa hali yako ya kutoweza kufikia na/au kutumia Tovuti ya Showmax, iwe kikamilifu au kabisa, ikiwa hutatii kifungu cha 6, 7 na 8 cha Vigezo vya Utumiaji.

3. Leseni na utumiaji unaoruhusiwa

3.1 Unaruhusiwa kufikia na kutumia Tovuti ya Showmax, au maelezo yoyote au vifaa vilivyotolewa kwenye Tovuti ya Showmax, kwa njia halali, kwa madhumuni yako binafsi na yasiyo ya kibiashara, na kulingana na Masharti ya Matumizi, na si kwa madhumuni ya kibiashara au mengineyo yasiyo binafsi, isipokuwa tu umepata idhini ya maandishi kutoka kwetu kabla.

3.2 Unaweza kuhifadhi ukurasa wa wavuti wa Tovuti ya Showmax mradi:

3.2.1 kusudi la kuhifadhi ni kuendelea kutazama maudhui kuanzia ulipoachia au kupakua maudhui kutoka kwenye Tovuti ya Showmax kwa urahisi zaidi;

3.2.2 hubadilishi, hutoi nakala, huathiri data au maudhui yaliyohifadhiwa kwa namna yoyote, au vinginevyo kutumia data au maudhui yaliyohifadhiwa kwa namna ambayo hatujaidhinisha katika Vigezo hivi vya Utumiaji; na

3.2.3 unasasisha au kuondoa data au maudhui yaliyohifadhiwa katika mfumo wa kompyuta yako iwapo tutakuomba uondoe.

3.3 Hakuna mtu yeyote anayepaswa kuonyesha maudhui ya tovuti nyingine katika Tovuti ya Showmax kwa namna yoyote bila idhini yetu ya mapema ya maandishi.

3.4 Isipokuwa kwa waendeshaji wa injini za utafutaji wa kweli na matumizi ya kifaa cha utafutaji kilichotolewa kwenye Tovuti ya Showmax, hakuna mtu anayeruhusiwa kutumia, au kujaribu kutumia, teknolojia au programu yoyote (kama vile wavamizi wa wavuti, mende wa wavuti, roboti, bots za kuvuna au skripu) kutafuta Tovuti ya Showmax kwa madhumuni yoyote bila idhini ya maandishi kutoka kwetu kabla.

3.5 Unaweza kuchapisha maoni, ujumbe na mawazo yako binafsi kwenye jukwaa lolote katika Tovuti ya Showmax baada ya kujisajili ili kushiriki katika utoaji maoni na/au ukadiriaji wa Huduma ya Showmax na umekubali vigezo na masharti ya jukwaa (ikiwa yapo).

3.6 Unajitolea kutohakikisha au kuweka taarifa yoyote au maudhui kwenye Tovuti ya Showmax ambayo: ni, au inaweza kuwa, kinyume cha sheria, ya kuashiria, inayoonea, isiyo ya adabu, ya kibinafsi, matangazo ya kibiashara, vifaa vya masoko, yenye lugha chafu, isiyo ya kweli, ya uongo, potofu, inayoongopea; inakiuka haki za faragha, haki za mali ya akili au haki nyingine yoyote au maslahi yetu, ya Washirika wetu au ya mtu wa tatu; au ni hatari kwa namna yoyote. Bila kudhibiti ujumla wa kifungu hiki, unakubali kuwa hutapakia, kuchapisha au vinginevyo kutuma maudhui yoyote yanayojumuisha yoyote yafuatayo:

3.6.1 maelezo yoyote binafsi yako au ya mtu mwingine;

3.6.2 taka au mawasiliano yasiyohitajika, ikiwa ni pamoja na matangazo ya tovuti na/au huduma zingine, barua za mfululizo, mipango ya ulaghai, kura za maoni au maombi;

3.6.3 kufurika bodi za jukwaa lolote kwa machapisho mengi kupita kiasi, machapisho yasiyo ya maana, machapisho yasiyohusiana na mada au machapisho ya maelezo yasiyohitajika;

3.6.4 mazungumzo ya kutoka nje ya mada, hayahusiani na utatuzi wa tatizo lililopo, yanajirudia au ni ya kampeni, yanayotangaza bidhaa au huduma kutoka kwa watoa huduma wengine, au yanatukana bidhaa au huduma yoyote ya kampuni;

3.6.5 malalamiko yasiyo na msingi au ya kuudhi kutuhusu sisi, Washirika wetu au sera au desturi zetu;

3.6.6 ushambuliaji (ikiwa ni pamoja na 'Uchochezi') wa Mtumiaji mwingine kwa namna ya kuchochea au kuendeleza mabishano au mgogoro; kuunda majina ya watumiaji ili kushambulia utambulisho wa Watumiaji wengine; kuiga watu wengine au kudanganya kuhusu utambulisho au mahitimu yako; machapisho yanayochapishwa chini ya majina ya ziada ya watumiaji au majina mengine ya utani kwa kusudi la kuunga mkono au kupaka wengine matope; machapisho yanayokiuka faragha ya Mtumiaji yeyote kwa kujumuisha maelezo binafsi ya Mtumiaji huyo;

3.6.7 kuchapisha kiungo au vinginevyo kuwaelekeza Watumiaji wengine kwenye maelezo au maudhui yoyote ambayo, yakichapishwa katika Tovuti ya Showmax yanaweza kukiuka Vigezo hivi vya Utumiaji;

3.6.8 URL za Tovuti za Washirika Wengine ambazo zinaweza kuwa na maudhui ya kukera au ya kinyume cha sheria;

3.6.9 ushauri unaoweza kusababisha ukiukaji wa dhamana zozote za bidhaa au vifaa vyetu;

3.6.10 ushauri unaoweza kusababisha ukiukaji wa makubaliano kati ya Showmax na wateja wa Huduma ya Showmax, yanayobainisha vigezo na masharti yanayompa mteja idhini ya kufikia na kutumia Huduma ya Showmax kwa kubadilishana na malipo ya ada husika ya usajili, au Masharti yoyote ya Ziada; na

3.6.11 ushauri ambao, ukifuatwa, unaweza kusababisha jeraha au madhara.

3.7 Tunaweza kudhibiti machapisho au mawasilino katika Tovuti ya Showmax ili kutoa uwasilishaji wenye mpangilio wa maelezo haya, ili kuhakikisha kuwa machapisho au mawasilisho yanatii Vigezo hivi vya Utumiaji, na kwa sababu nyingine yoyote tunayozingatia kuwa inafaa, ingawa hatutakuwa na wajibu wa kufanya hivyo.

3.8 Tunaweza kubadilisha, kukataa kuchapisha au kuondoa maudhui yoyote uliyochapisha, ingawa hatutakuwa na wajibu wa kufanya hivyo.

3.9 Unahimizwa kuripoti kwetu maelezo au maudhui yaliyo kwenye Tovuti ya Showmax ambayo unaamini kuwa yanakiuka wajibu wetu uliobainishwa katika Vigezo hivi vya Utumiaji.

3.10 Ili kudhibiti Tovuti ya Showmax vizuri, tunaweza kuwateua wafanyakazi au watu wengine kutenda kama wadhibiti na wasimamizi wa Tovuti ya Showmax ("Wadhibiti"). Unakubali kutii maagizo yetu au ya Wadhibiti kuhusu ufikiaji na utumiaji wako wa Tovuti ya Showmax.

3.11 Hatuwajibiki kwa maelezo au maudhui yoyote unayochapisha au yanayochapishwa na washirika wengine katika Tovuti ya Showmax.

3.12 Ikiwa utaweka taarifa yoyote au maudhui kwenye Tovuti ya Showmax, utawajibika kwa kupotea, dhima au uharibifu wowote ambao sisi au Washirika wetu tunaweza kupata, moja kwa moja au kwa njia ya moja kwa moja, kutokana na machapisho yako kwenye Tovuti ya Showmax.

4. Gharama ya utumiaji wa Tovuti ya Showmax

4.1 Kwa kutegemea Vigezo hivi vya Utumiaji, unaweza kutumia Tovuti hii ya Showmax bila kulipia. Hata hivyo, ufikiaji wa baadhi au kurasa zote katika Tovuti ya Showmax unaweza kuruhusiwa tu kwa watu ambao wamejisajili kufikia kurasa zilizozuiwa katika Tovuti ya Showmax kwa kufungua Akaunti ya Showmax.

4.2 Licha ya kifungu cha 4.1, tunaweza baadaye kukutoza ili kufikia na/au kutumia Tovuti ya Showmax, au kipengele chake chochote, mradi tutakupa taarifa mapema kuhusu mabadiliko hayo katika Tovuti ya Showmax.

5. Viungo

5.1 Kwa kutegemea Vigezo hivi vya Utumiaji, unaweza kuunganisha Tovuti ya Showmax kutoka kwenye tovuti nyingine.

5.2 Unapounganisha Tovuti ya Showmax kutoka kwenye tovuti nyingine, unafanya hivyo kwa tahadhari yako binafsi.

5.3 Tunaweza kutoa viungo vya tovuti ambazo hatuzimiliki na/au hatuzidhibiti ("ovuti za Washirika Wengine"). Viungo hivyo havimaanishi kuwa tunaidhinisha, tunakubaliana au tunaunga mkono maelezo au maudhui ya Tovuti hizo za Washirika Wengine.

5.4 Hatuna uwezo wa kudhibiti kihariri maelezo au maudhui yaliyo kwenye Tovuti hizo za Washirika Wengine na wala sisi au mtu mwingine yeyote tunayemdhibiti au anayetudhibiti ("Mshirika") hatawajibika kwa namna yoyote kwa ufikiaji au kutoweza kufikia Tovuti hizo za Washirika Wengine, au kwa maelezo au maudhui yoyote yanayotolewa kwenye au kupitia Tovuti hizo za Washirika Wengine, au kwa hasara, dhima au uharibifu wowote wa mali unaoweza kupata kutokana na ufikiaji wa Tovuti ya Mshirika Mwingine kupitia kiungo katika Tovuti ya Showmax.

6. Usalama

6.1 Hupaswi, kufanya au kutofanya kimakusudi au kizembe kitu chochote cha kuathiri au kuvuruga Tovuti ya Showmax, au kuathiri usalama au uthabiti wa Tovuti ya Showmax, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, kwa kuwasilisha au kujaribu kuwasilisha msimbo wowote hasidi (kama vile virusi vya kompyuta, vidudu na virusi vya trojan horse) au kipengele kingine hasidi au haribifu katika Tovuti ya Showmax, au seva na mtandao wa kompyuta unaoendesha Tovuti ya Showmax.

6.2 Unawajibika kwa usalama na utumiaji unaofaa wa jina lako la mtumiaji na nenosiri.

6.3 Ni lazima uchukue hatua zote zinazofaa iwezekanavyo kuzuia kuathiriwa kwa usalama na uthabiti wa Tovuti ya Showmax.

7. Faragha

7.1 Sera ya Faragha inabainisha maelezo yako binafsi tunayokusanya unapotumia Tovuti ya Showmax, jinsi tunavyokusanya maelezo yako binafsi, sababu ya kuyakusanya na jinsi tunavyoyatumia na masuala yanayohusiana. Tafadhali soma Sera ya Faragha kwa umakini ili uelewe mitazamo na desturi zetu kuhusu maelezo yako binafsi na jinsi tunavyoyashughulikia (hata kama wewe ni mtumiaji wa muda mrefu wa tovuti) na uwasiliane nasi iwapo unahitaji ufafanuzi au usaidizi.

7.2 Vigezo vya Sera yetu ya Faragha vimejumuishwa katika Vigezo hivi vya Utumiaji, na unakubali kufuata Sera ya Faragha kana kwamba masharti yake yamejumuishwa kikamilifu katika Vigezo hivi vya Utumiaji.

8. Haki za mali ya uvumbuzi na utumiaji wa jina la kikoa

8.1 Mali yote ya uvumbuzi katika Tovuti ya Showmax, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu programu, maelezo, maudhui, vipengele vya muundo, hifadhidata, maandishi, picha, michoro, nembo, majina ya biashara, alama za huduma, viungo na jina/majina ya vikoa, iwe yamesajiliwa au hayajasajiliwa ("Mali ya Uvumbuzi") ni mali ya, au leseni yake imekabidhiwa kwetu na/au Washirika wetu.

8.2 Hupaswi kuchukulia Vigezo hivi vya Utumiaji kama hatua ya kupewa leseni au haki yoyote ya kutumia Mali ya Uvumbuzi bila idhini yetu ya mapema ya maandishi.

8.3 Unakubali hasa kuwa hutanakili, kutoa upya, kubadilisha, kufanya utafiti wa kihandisi, kuiga, kuchapisha, kuuza, kusambaza, kutuma, kutangaza, kueneza, kutumia vibaya au kutumia Mali ya Uvumbuzi au kipengele chake chochote kwa njia yoyote ya kinyume cha sheria.

8.4 Tumehifadhi Haki zetu zote za Mali ya Uvumbuzi.

9. Makanusho

9.1 Marejeleo ya Showmax, "sisi", au "nasi" inajumuisha wakurugenzi, maofisa, wafanyakazi, maajenti, wawakilishi, mawakala na Washirika.

9.2 Maelezo, mawazo na maoni yanayotolewa katika Tovuti ya Showmax hayapaswa kuzingatia kuwa ni ushauri wetu wa kitaalamu au maoni rasmi, na unahimizwa kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kuchukua hatua yoyote kuhusiana na maelezo, mawazo au maoni yaliyotolewa katika Tovuti ya Showmax.

9.3 Kadri inavyoruhusiwa na sheria inayotumika:

9.3.1 Hatutoi mahakikisho na hatutoi dhamana, iwe moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kuhusu Tovuti ya Showmax au maelezo yanayotolewa katika Tovuti ya Showmax, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, hatutoi mahakikisho na hatutoi dhamana:

9.3.1.1 kuwa Tovuti ya Showmax itaboreshwa ili kutimiza mahitaji au matarajio yako binafsi;

9.3.1.2 kuhusu wakati ambapo Tovuti ya Showmax itasasishwa, au kuwa huduma ya Tovuti ya Showmax haitakatizwa au haitakuwa na hitilafu; au

9.3.1.3 kuwa maelezo yanayotolewa katika Tovuti ya Showmax yatakuwa ya kweli, kamili, sahihi au ya kutegemewa.

9.3.2 Hatutawajibika na tunakana dhima yote ya hasara, uwajibikaji, jeraha, gharama au uharibifu wowote (iwe wa moja kwa moja, usio wa moja kwa moja, wa kiajali, wa adhabu au unaombatana) wa namna yoyote, unaotokana na uzembe, na unaompata mtu yeyote anayefikia, anayetumia au anayetegemea Tovuti ya Showmax. Bila kudhibiti ujumla wa kifungu hiki, hatutawajibika kwa hasara, dhima au uharibifu wowote wa namna yoyote unaompata mtu yeyote na unaotokana moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na:

9.3.2.4 ufikiaji wa Tovuti ya Showmax;

9.3.2.5 kutoweza kufikia au kucheleweshwa au kutatizika kufikia Tovuti ya Showmax, kwa kiwango ambacho hali hiyo ya kutoweza kufikia, kucheleweshwa au kutatizika kufikia inatokana na sababu ambazo hatuna uwezo wa kuzidhibiti;

9.3.2.6 ufikiaji wa tovuti zozote zilizounganishwa na Tovuti ya Showmax;

9.3.2.7 kutoweza kufikia, kucheleweshwa au kutatizika kufikia tovuti zozote zilizounganisha na Tovuti ya Showmax;

9.3.2.8 ufikiaji, utumiaji au utegemeaji wa maelezo au maudhui yanayopatikana katika Tovuti ya Showmax;

9.3.2.9 maudhui yoyote yaliyochapishwa na washirika wengine katika Tovuti ya Showmax;

9.3.2.10 huduma zinazopatikana katika Tovuti ya Showmax;

9.3.2.11 hali yetu ya kuchelewa au kutoweza kutimiza wajibu wetu chini ya Vigezo hivi vya Utumiaji kwa kiwango ambacho hali hiyo ya kuchelewa au kutoweza kutimiza wajibu inatokana na sababu ambazo hatuna uwezo wa kuzidhibiti; au

9.3.2.12 kitendo chochote cha kizembe au usahaulifu wetu au wa washauri wetu, maajenti au wafanyakazi.

10. Maelezo ya bidhaa na mabadiliko yanayofanywa

10.1 Kabla ya kufanya maamuzi yoyote au kuingia katika mikataba au kufanya malipo, unapaswa kuthibitisha maelezo yanayohusika, kama vile hali, maelezo, maudhui na gharama ya bidhaa na huduma (k.m., ada ya usajili au kifaa) kupitia Tovuti ya Showmax.

10.2 Tunakufahamisha pia kuwa bidhaa na huduma zetu (na kipengele chochote, ikiwa ni pamoja na hali, maudhui, vipengele na bei) zinaweza kubadilika mara kwa mara. Maelezo yaliyosasishwa yatachapishwa katika Tovuti ya Showmax Website mara kwa mara.

11. Bei

11.1 Bei za bidhaa na huduma mbalimbali tunazotoa hubainishwa katika Tovuti ya Showmax na zinaweza kubadilika. Tutachapisha bei zilizosasishwa katika Tovuti ya Showmax mara kwa mara.

11.2 Marejeleo ya "bei ya usajili" au "ada ya usajili" katika Tovuti ya Showmax inamaanisha ada ya usajili, ikiwa ni pamoja na VAT, lakini bila kujumuisha kifaa chochote kinachotumika kufikia Huduma ya Showmax.

12. Wakati, mahali, namna na sifa za Ujumbe wa Data

12.1 Washirika wanakubali yafuatayo:
unayotutumia itachukuliwa kuwa tumeipokea iwapo tu tutajibu au kuthibitisha kuwa tumeipokea;

12.1.2 Ujumbe wa Data tunaokutumia utachukuliwa kuwa umeupokea wakati data kamili ya ujumbe inaingia katika mfumo wa habari ulioweka au unaotumia kwa kusudi hilo na unaweza kuirejesha na kuichakata;

12.1.3 Ujumbe wa Data unaotutumia au tunaokutumia utachukuliwa kuwa umetungwa na kutumwa kutoka eneo lolote ambako Showmax inafanya kazi;

12.1.4 Njia za uthibitishaji kama vile saini za kielektroniki au mbinu za usimbaji fiche hazihitajiki kwa makusudi ya mawasiliano kati yako nasi;

12.1.5 Ujumbe wowote wa Data unaotutumia kutoka kwenye kompyuta, anwani ya IP au kifaa cha mkononi unachomiliki au unachotumia kwa kawaida utachukuliwa kuwa umetumwa kwetu kutoka kwako, au kwa niaba yako na mtu uliyempa idhini ipasavyo.

13. Marekebisho ya Tovuti ya Showmax na Vigezo vya Utumiaji

13.1 Unakubali kuwa tunaweza kubadilisha au kukomesha maelezo, maudhui, huduma, programu au kipengele kingine chochote cha Tovuti ya Showmax, na kubadilisha Vifaa vya Teknolojia ya Mawasiliano vinavyohitajika kufikia na kutumia Tovuti ya Showmax au maelezo, maudhui, huduma na programu katika Tovuti ya Showmax.

13.2 Mabadiliko hayo hayataathiri haki na wajibu wako kuhusiana na shughuli ya malipo au makubalino kati yetu ambayo tayari yamekamilika kufikia wakati wa mabadiliko hayo.

13.3 Ruhusa zote zinazotolewa katika Vigezo hivi vya Utumiaji zinatolewa kwa msingi wa ruhusa zisizo za kipekee na zisizoweza kuhamishwa.

13.4 Tunaweza kurekebisha Vigezo hivi vya Utumiaji wakati wowote.

13.5 Tutakufahamisha kuhusu mabadiliko hayo angalau kwa kukutumia barua pepe, kupitia taarifa ibukizi unapofikia Tovuti ya Showmax, au kupitia taarifa ibukizi unapoingia katika Akaunti yako ya Showmax.

13.6 Iwapo hukubali mabadiliko yoyote yaliyofanywa katika Vigezo hivi vya Utumiaji, unaweza kukomesha utumiaji wako wa Huduma ya Showmax kwa njia iliyoelezwa katika Makubaliano kati yako na Showmax.

13.7 Iwapo kutakuwa na tofauti au mvutano kati ya Vigezo hivi vya Utumiaji na vigezo na masharti mengine yoyote yanayohusiana na bidhaa au huduma nyingine inayotolewa na Showmax au mshirika mwingine, masharti yaliyo katika Vigezo hivi vya Utumiaji yatatumika kuhusiana na Huduma ya Showmax na vigezo na masharti mengine yatatumika kuhusiana na bidhaa au huduma hiyo nyingine.

14. Kukomeshwa kwa huduma ya Tovuti ya Showmax

14.1 Tunaweza kukomesha huduma ya Tovuti ya Showmax, au kipengele chake chochote wakati wowote.

14.2 Sera yetu ya Faragha, kuhusiana na Mali yetu ya Uvumbuzi itaendelea kutumika endapo Vigezo hivi vya Utumiaji vitakomeshwa kwa sababu yoyote ile.

15. Makubaliano yote na mabadiliko

15.1 Vigezo hivi vya Utumiaji, kama tunavyovirekebisha mara kwa mara, vinaunda makubaliano yote kati yetu nawe kuhusiana na suala husika na yanapewa kipaumbele kuliko makubaliano yoyote ya awali kati yako nasi.

15.2 Iwapo sharti lolote lililoelezwa hapa litapatikana kuwa haliwezi kutekelezwa au si sahihi kwa sababu yoyote, vigezo na masharti hayo yatatengwa na vigezo na masharti yaliyobaki, na vigezo na masharti yaliyobaki yataendelea kutekelezwa na kutumika.

16. Mawasiliano

Unapojisajili katika Tovuti ya Showmax, tutakagua mifumo yetu ili kuthibitisha iwapo umeomba kutopokea mawasiliano kutoka kwetu kuhusu bidhaa na/au huduma zetu. Iwapo hungependa kupokea mawasiliano hayo kutoka kwetu, tafadhali rejelea "sehemu ya akaunti" katika Tovuti ya Showmax au tumia chaguo za "jiondoe" zilizowekwa katika mawasiliano ya matangazo ya moja kwa moja tunayokutumia.

17. Gharama za kisheria

Hatutawajibika kwa gharama zozote unazoingia za kupata ushauri wa kitaalamu kuhusiana na Vigezo hivi vya Utumiaji.

18. Ukiukaji

18.1 Bila kuhujumu haki zetu zingine zozote, tunaweza kudai fidia kutoka kwa mtu yeyote anayekiuka Vigezo hivi vya Utumiaji, na kusababisha tupate hasara, tudaiwe, madhara au uharibifu wa mali.

18.2 Utepetevu au ulegevu tunaoweza kukuonyesha mara kwa mara au mshirika asipotekeleza au kutumia haki au sharti lolote la Vigezo hivi vya Utumiaji si kitendo cha kuhujumu na si uachiliaji wa haki au sharti lolote katika Vigezo hivi vya Utumiaji au sheria yoyote inayotumika. Hakuna kitendo cha uachiliaji wa haki au masharti kitakachotumika isipokuwa ibainishwe moja kwa moja kuwa ni kitendo cha uachiliaji na umefahamishwa kwa maandishi.