Ili kudhibiti vifaa vyako, kwanza nenda kwenye kichupo cha Vifaa katika Akaunti yako:
- Nenda kwenye Showmax.com na uingie kwenye akaunti.
- Nenda kwenye Akaunti kupitia upau wa menyu wa juu kulia.
- Chagua Vifaa.
- Hapa utapata orodha ya vifaa vyako vyote vilivyosajiliwa.
Badilisha majina ya vifaa vyako
- Bofya chaguo la Badilisha Jina karibu na kifaa unachotaka kubadilisha.
- Badilisha jina la kifaa, kisha ubofye kitufe cha Badilisha Jina ili kuhifadhi jina.
Ondoka kwenye vifaa vyote
Katika sehemu ya Vifaa Vingine, chagua Ondoka Kwenye Vyote ili uondoke kwenye vifaa vyako vyote
Ondoa vifaa vilivyosajiliwa
Vifaa vitaondolewa kiotomatiki kwenye Akaunti yako ya Showmax utakapofikisha kikomo cha vifaa 10, unapoongeza vifaa vipya. Kwa sasa hakuna chaguo la kuondoa vifaa kibinafsi.
Weka vifaa vipya
Ingia tu kwenyeshowmax.com au programu ya Showmax kutoka kwa kifaa kipya na itaongezwa kiotomatiki kwenye Akaunti yako ya Showmax.