Je, unatatizika kuingia kwenye Showmax? Angalia Nitafuata hatua gani ili niingie kwenye akaunti yangu ya Showmax?Fuata hatua zilizo hapa chini za utatuzi ili ujaribu kurudi kwenye Akaunti yako:
Angalia ikiwa ulimaliza kujisajili
Iwapo ulianza kujisajili kwenye Showmax, lakini hukukamilisha hatua zote au hukupokea uthibitisho wa barua pepe kutoka kwetu, huenda ukahitajika kukamilisha kujisajili kabla ya kuingia. Ili upate usaidizi zaidi wa kujisajili, angalia Kutatua matatizo unapojisajili kwenye Showmax.
Hakikikisha unatumia kifaa kinachoruhusiwa
Angalia Ni vifaa gani vinaweza kutumia Showmax? ili uangalie ikiwa kifaa chako kinaendana na Showmax na upate usaidizi wa kifaa mahususi.
Thibitisha anwani yako ya barua pepe na nambari ya simu
Ikiwa unaweza kuingia kwenye Showmax.com, lakini si kwenye programu ya Showmax, huenda ukahitaji kuthibitisha anwani ya barua pepeau namba ya simu ya mkononi.
Angalia vitambulisho ya Akaunti yako
Makosa ya tahajia hutokea! hakikisha umeweka anwani yako ya barua pepe au nambari ya simu ya mkononi, na nenosiri kwa usahihi.
Iwapo bado huwezi kuingia, jaribu kuweka upya nenosiri lako au kuingia ukitumia namba yako ya simu ya mkononi badala ya anwani ya barua pepe yako, au ikiwa huwezi kukumbuka vitambulishi vyako, angalia Nitapataje Akaunti ya Showmax iliyopotea?
Iwapo unashuku kuwa kulikuwa na makosa ya kuandika barua pepe au nambari yako ya simu ulipojiandikisha, tafadhali Wasiliana Nasi ili tukusaidie zaidi.