Utaratibu huu unatofautiana kulingana na muundo na umbo la TV Mahiri yako.
Samsung Smart TV
- Nenda kwenye samsung.com.
- Weka nambari ya muundo wa TV yako kwenye kisanduku cha kutafutia, kwa mfano ES6600.
- Chagua muundo wako kwenye matokeo ya utafutaji.
- Kwenye ukurasa wa maelezo ya bidhaa, sogeza chini hadi sehemu ya Usaidizi (au Programu ya Ulinzi).
- Fungua Mwongozo wa Kuboresha upate maagizo ya kuboresha TV yako.
Njia rahisi zaidi ni njia ya mtandaoni, Vinginevyo fuata mbinu ya kusasisha USB.
Televisheni Mahiri ya LG
- Nenda kwenye lg.com.
- Weka nambari ya muundo wa TV yako kwenye kisanduku cha kutafutia, kwa mfano 65LB720T.
- Chagua muundo wako kwenye matokeo ya utafutaji.
- Kwenye ukurasa wa maelezo ya bidhaa, chagua kitufe cha Usaidizi wa Bidhaa.
- Chagua kichupo cha Usasishaji wa Programu.
- Fungua Mwongozo wa Kuboresha Programu na ufuate maagizo husika.
Televisheni Mahiri ya Hisense
Kwenye Hisense Smart TV yako, chagua Mipangilio > Kuhusu > Sasisho la Mfumo > Angalia Uboreshaji wa Programu ya Ulinzi.
Teua kitufe cha Tambua ili uangalie masasisho yanayopatikana.