Maudhui ya Showmax yanapatikana katika HD kamili (1080p). Teknolojia yetu ya utiririshaji kulingana na mahitaji inamaanisha kwamba unapaswa kupata ubora wa hali ya juu zaidi unaopatikana kwa kasi ya muunganisho wako na kifaa kiotomatiki, lakini ikiwa huduma si nzuri inavyopaswa, basi jaribu kufuata hatua zilizo hapa chini za utatuzi.
Kagua mtandao wako
Showmax hujibadilisha kiotomatiki kulingana na kasi ya muunganisho wako wa intaneti, ili kuhakikisha kuwa unaweza kuendelea kutazama. Maudhui yanaweza kutiririka kwa ubora wa chini kwenye miunganisho ya polepole au isiyo thabiti ya intaneti.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu mahitaji ya mtandao, angalia Je, Intaneti yangu inahitaji kuwa na kasi kiasi gani ili utumie Showmax?
Kagua vifaa vyako
Ili upate ubora wa hali ya juu zaidi unaopatikana, maunzi yote unayotumia sharti yaruhusu. Hii ina maana kwamba pamoja na kifaa chako, vifuasi vyote (k.m. nyaya za HDMI, vionyesho vilivyounganishwa na vidhibiti, na kitu kingine chochote kinachotumika) lazima pia viwiane na DRM na HDCP.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu mahitaji ya kifaa, angalia Mahitaji ya HDCP kwenye kifaa changu ni yepi?
Angalia Mipangilio yako ya Data
Showmax hukusaidia kuendelea kudhibiti matumizi yako ya data kwa kubadilisha ubora wa utiririshaji. Ikiwa huridhiki, jaribu kuongeza ubora wa utiririshaji katika Akaunti yako.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubadilisha ubora wako wa utiririshaji, angalia Je, ninawezaje kudhibiti mipangilio yangu ya data ya utiririshaji?