Kituo cha Usaidizi

Ninapokea ujumbe wa hitilafu ukisema kuwa Showmax haipatikani kwenye nchi yangu


Ikiwa uko katika nchi ambayo Showmax inapatikana na upokee hitilafu inayosema huduma hii haipatikani kwenye nchi yako, inamaanisha kuwa hatuwezi kubainisha kwa usahihi mahali ulipo. 

 

Hili linaweza kutokea ikiwa eneo la kijiografia la anwani ya IP unayotumia linahusishwa na nchi tofauti na ile uliyomo. Ukaribu wa mpaka wa nchi jirani unaweza pia kuwa sababu. 

 

Angalia hatua zifuatazo za utatuzi ili ujaribu kurekebisha suala hilo:

  • Hakikisha kuwa huduma za DNS au VPN (k.m. UnoTelly) zimezimwa.
  • Hakikisha kwamba huduma mbadala za ubanaji (k.m. Google Data Saver) zimezimwa.
  • Jaribu kuunganisha kwenye Wi-Fi, au chanzo tofauti cha Wi-Fi.
  • Wasiliana na Mtoa Huduma wako wa Mtandao (ISP) ili uthibitishe eneo kamili la anwani yako ya IP.

Je, maoni haya yamekufaa?