HDCP ni nini?
HDCP inamaanisha Ulinzi wa Maudhui Dijitali ya Kiwango cha Juu cha Masafa. HDCP hulinda maudhui dijitali yenye hakimiliki yakitumwa kutoka kwenye kifaa hadi runinga yako.
DRM ni nini?
DRM inamaanisha Usimamizi wa Haki za Kidijitali DRM ni matumizi ya teknolojia kudhibiti na kusimamia ufikiaji wa nyenzo zilizo na hakimiliki.
Showmax hutumiaje HDCP na DRM?
Showmax imetekeleza masharti ya HDCP na DRM ili kulinda maudhui yake yenye hakimiliki.
Mahitaji ya HDCP na DRM yatatumika kwa vituo na matukio yote ya moja kwa moja, VoD na maudhui ya nje ya mtandao (vipakuliwa) yanayotolewa na watoa huduma wa nje kama vile studio za Hollywood.
Kwenye Showmax Originals au maudhui yanayomilikiwa na kikundi, huenda tukatumia sheria za ulinzi zisizo kali sana.
Ninahitaji nini ili nitazame maudhui yenye mahitaji ya HDCP na DRM?
Utahitaji maunzi yanayoendana na DRM na HDCP ili ufurahie maudhui yetu. Ili kupata maelezo zaidi, angalia Mahitaji ya DRM na HCDP kwenye kifaa chako.