Kituo cha Usaidizi

Ulinzi wa Maudhui Dijitali wa Kiwango cha Juu cha Masafa ni nini?


HDCP inamaanisha Ulinzi wa Maudhui Dijitali ya Kiwango cha Juu cha Masafa. Showmax imetekeleza masharti ya HDCP na DRM ili kulinda maudhui yake yenye hakimiliki.

Hii ina maana kwamba utumiaji wa maunzi ya DRM na HDCP unaweza kuhitajika unapotazama maudhui yote au baadhi ya maudhui yetu.

Maana yake ni kwamba ubora wa kawaida utakuwa mpangilio chaguo-msingi wa vifaa ambapo DRM ya programu pekee ndiyo inayotumika.

Ubora wa HD unawezekana ikiwa HDCP inatumika kwenye kifaa, kebo na vionyesho vya nje vilivyounganishwa.

Ubora wa FullHD unapatikana kwa vifaa vilivyo na DRM ya maunzi na usaidizi wa HDCP.

Mahitaji ya HDCP yatatumika kwa vituo na matukio yote ya moja kwa moja, VoD, na maudhui ya nje ya mtandao (vipakuliwa) vinavyotolewa na watoa huduma wa nje kama vile studio za Hollywood.

Kwenye Showmax Originals au maudhui yanayomilikiwa na kikundi, tunaweza kutumia sheria kali za ulinzi ili kuyatoa katika hali ya ubora zaidi


Je, maoni haya yamekufaa?