Showmax ina idadi ya vipengele vya kukusaidia kuweka kikomo cha data unayotumia kutiririsha.
Kudhibiti mipangilio yako ya data
Unaweza kuweka kikomo cha data inayotumika kwa saa moja ya kutiririsha au kudhibiti utiririshaji kwenye Wi-Fi ndani ya Akaunti yako pekee. Ili upate maelezo zaidi, angalia Ninadhibiti vipi mipangilio yangu ya utiririshaji data?
Kutumia vipakuliwa
Programu ya Showmax hukuruhusu kupakua maudhui ukiwa kwenye Wi-Fi, ili kutazama baadaye wakati haupo. Ili upate maelezo zaidi, angalia Jinsi ya kupakua maudhui kwenye kifaa chako.