Kituo cha Usaidizi

Je, ninawezaje kudhibiti mpangilio yangu ya data ya utiririshaji?


Unaweza kudhibiti matumizi yako ya data na kuweka kikomo cha ubora wa utiririshaji kwenye ukurasa wa Mipangilio ya Data katika programu ya Showmax.

 

Ili kufikia ukurasa wa Mipangilio ya Data:


1. Ingia kwenye programu ya Showmax
2. Chagua Akaunti kwenye upau wa menyu.
3. Chagua Mipangilio.
4. Chagua Mipangilio ya Data.

 

Matumizi ya data

Kwa chaguomsingi, utaweza kutiririsha kwa kutumia data ya mtandao wa simu na kwenye Wi-Fi.

Unaweza kuzuia utiririshaji kwa Wi-Fi pekee kwa kubadilisha kigeuza katika Mipangilio ya Data katika programu ya Showmax.

 

Ubora wa utiririshaji

Kwa chaguomsingi, utiririshaji utakuwa hadi kasi ya 240 MB/h.

Unaweza kubadilisha hili kuwa chaguo ambalo linafaa mpango wako wa data, kwa kuchagua kutoka kwa chaguo katika Mipangilio ya Data kwenye programu ya Showmax.


Je, maoni haya yamekufaa?