Fuata hatua hizi ikiwa unaweza kuingia katika akaunti yako ya Showmax na ungependa kubadilisha nenosiri lako:
- Ingia kwenye akaunti yako ya Showmax.
- Nenda kwenye Mipangilio na uchague Badilisha Nenosiri. Chagua Endelea.
- Angalia barua pepe zako upokee maelekezo kuhusu jinsi ya kubadilisha nenosiri lako.
- Fuata maelekezo yaliyo katika barua pepe ili kubadilisha nenosiri lako na kulihifadhi.
Ikiwa umepoteza uwezo wa kuingia katika akaunti yako, fuata maelekezo yaliyo hapa ili uweke nenosiri lako.
Vidokezo vya kuweka nenosiri thabiti
Hivi hapa vidokezo vya kuweka nenosiri thabiti:
- Weka nenosiri la urefu wa angalau herufi 10.
- Tumia mchanganyiko wa herufi, nambari, herufi kubwa na herufi maalum.
- Usiweke taarifa za kibinafsi na majina halisi.
- Kumbuka, nenosiri lisilo rahisi litakuwa thabiti zaidi.
Ikiwa unahitaji usaidizi zaidi wa kuingia, tafadhali wasiliana nasi.