Vifuatavyo ni baadhi ya vigezo vinavyoweza kukuwezesha kurejeshewa pesa za mpango wako wa Showmax:
- Umefungua akaunti mbili zilizo na maelezo sawa ya malipo, na akaunti moja haijawahi kutumika kutiririsha.
- Showmax ilikutoza kwa njia isiyo sahihi, kwa mfano:
- Kutozwa mara mbili.
- Kutoza kiasi kisicho sahihi.
- Kutoza tarehe zisizo sahihi.
- Kutoza bila kupeana usajili.
- Iwapo unaweza kuthibitisha kwamba ulighairi au uliomba kughairi usajili kwa wakati, na ombi hili halikuchakatwa, na kwamba pia hakujawa na shughuli zozote za kutazama maudhui kwenye akaunti.
- Ulistahiki kupata ofa kulingana na vigezo vya ofa, lakini hukupata ofa hiyo.
Ili kupata maelezo kuhusu jinsi ya kuomba kurejeshewa pesa, angalia Utaratibu wa ombi la kurejeshewa pesa ni gani?