Ili kuomba kurejeshewa pesa kwenye Showmax, unahitaji kufuata mchakato ulio hapa chini:
1. Angalia makala ya Mchakato wa kurejeshewa pesa kwenye Showmax uone kama unastahiki kuporejeshewa pesa.
2. Wasiliana na Timu yetu ya Usaidizi kwa Wateja upate usaidizi wa kuomba kurejeshewa pesa.
Timu hii:
1. Italikagua ombi lako la kurejeshewa pesa.
2. Italituma ombi lako la kurejeshewa pesa kwa uchunguzi zaidi ikihitajika.
3. Itaidhinisha ombi lako la kurejeshewa pesa, kulingana na matokeo ya uchunguzi.
Huenda pesa zitarejeshwa katika akaunti yako kati ya siku 7-14 za kazi baada ya kuidhinishwa.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu hili tafadhali wasiliana nasi.