Kituo cha Usaidizi

Nitaghairi vipi usajili wangu wa Showmax?


Kuna njia tofauti za kughairi usajili wako wa Showmax, kulingana na jinsi ulivyojisajili mwanzoni.  

 

Nilijisajili kwenye tovuti ya Showmax. 


Ikiwa umejisajili moja kwa moja kupitia tovuti yetu ya showmax.com, na unataka kughairi usajili wako wa Showmax, unaweza kufanya hivyo wakati wowote mtandaoni. Fuata hatua hizi rahisi: 

 

1. Ingia katika tovuti ya Showmax.
2. Chagua Akaunti kwenye upau wa menyu wa juu.
3. Chagua Mipango na Malipo.
4. Chagua Dhibiti Mpango.
5. Chagua Ghairi Mpango. 

 

Ni muhimu kutambua kwamba huwezi kughairi usajili wako wa Showmax kupitia programu kwa kuwa ni tofauti na iliyo kwenye app store. 

 

Nilijisajili kupitia mtoa huduma mshirika. 

 


Ikiwa ulijisajili kupitia mtoa huduma wa eneo lako, utahitaji kughairi usajili wako moja kwa moja kwenye huduma yake.

 


Je, maoni haya yamekufaa?