Kituo cha Usaidizi

Je, ninaweza kufutaje akaunti na data yangu ya Showmax?


Fomu ya Kuomba Data ya Showmax

Kwa maombi yoyote yanayohusiana na akaunti na data ya Showmax, unaweza kujaza f fomu yetu ya Kuomba Data ya Showmax
 
Kwa kutumia fomu yetu ya Kuomba Data ya Showmax, unaweza kuomba:
  • Kufuta data yako ya binafsi
  • Kufikia data yako ya binafsi
  • Kuhamisha data yako ya binafsi
Usijali, maombi yote yatachakatwa kupitia mfumo salama wa kiotomatiki. Tutakuarifu pindi tu tutakapopokea ombi lako.
 

Mchakato wa kufuta data

Iwapo umetuomba kufuta akaunti yako ya Showmax, tutakutumia taarifa kuhusu hatua za ombi lako kupitia barua pepe. 
 
Kwa vile data ni nyeti, tutahitaji kuthibitisha utambulisho wako kabla ya kuendelea na ombi lako la data. Ikiwa unatuma ombi kwa niaba ya mtu mwingine, tutahitaji uthibitisho kwamba una idhini yake.
 

Kumbuka kughairi usajili wako kwenye Showmax

Kufuta taarifa zako pekee hakuwezi kusimamisha malipo yoyote ya siku zijazo, ikiwa ni pamoja na gharama za kulipia usajili kiotomatiki. Ni wajibu wako kukagua, kudhibiti na kughairi majukumu yako ya malipo. Kwa mfano, ikiwa usajili wako utatozwa kupitia kampuni nyingine kama vile Apple au Google Play Store, bado unaweza kutozwa.
 
Angalia makala yetu kuhusu Nitafanya nini Kughairi usajili wangu wa Showmax? ili upate maelezo ya kina.
 
Pia, hakikisha unakagua Sheria na Masharti yetu ya Showmax.

Je, maoni haya yamekufaa?