Unaweza kusasisha anwani yako ya barua pepe ya Showmax mtandaoni kwa kuingia kwenye akaunti yako. Fuata tu hatua zinazofuata hapa:
- Nenda kwenye 'Mipangilio' na ubofye 'Sasisha anwani ya barua pepe'.
- Angalia barua pepe zako upate maelekezo kutoka kwetu kuhusu jinsi ya kubadilisha anwani yako ya barua pepe.
- Bofya kitufe cha 'Badilisha anwani ya barua pepe'.
- Weka anwani ya barua pepe yako mpya na ubofye 'Sasisha anwani ya barua pepe'.
Tutakutumia barua pepe nyingine ili kuthibitisha anwani yako mpya ya barua pepe. Fuata maagizo ya barua pepe ili kuthibitisha anwani yako ya barua pepe ya Showmax.
Ikiwa ulifanya makosa katika anwani ya barua pepe yako ya Showmax, wasiliana nasi na tutakusaidia kuirekebisha.