Kituo cha Usaidizi

Nitafanya nini nithibitishe anwani yangu ya barua pepe ya Showmax?


Kuthibitisha anwani yako ya barua pepe ya Showmax ndiyo njia bora zaidi ya kuthibitisha kwamba barua pepe zote muhimu za huduma zinaingia kwenye kikasha chako na kwamba akaunti yako iko salama. 

 

Fuata hatua hizi ili kuthibitisha anwani yako ya barua pepe ya Showmax

 

  1. Nenda kwenye Showmax.com kisha uingie kwenye akaunti.
  2. Nenda kwenye Akaunti kupitia upau wa menyu wa juu kulia.
  3. ChaguaMipangilio.
  4. Unapaswa kuona ujumbe juu ya ukurasa unaokuuliza Uthibitishe anwani yako ya barua pepe. Bofya Thibitisha.
  5. Nenda kwenye kikasha chako na utafute barua pepe inayokuomba Thibitisha anwani yako ya barua pepe ya Showmax.
  6. Bofya kitufe cha Thibitisha Anwani ya Barua pepe. 

Je, maoni haya yamekufaa?