Kituo cha Usaidizi

Nitatozwa lini kwa usajili wangu wa Showmax?


Tunachukua maelezo yako ya malipo unapojisajili kwenye Showmax. Ikiwa umechagua njia ya malipo ya kila mwezi inyorudiwa, tarehe utakapojiandikisha itakuwa tarehe yako ya malipo kila mwezi. 

K.m. Ikiwa ulijisajili kwenye Showmax tarehe 10, utatozwa tarehe 10 ya kila mwezi.

 

Hali tofauti pekee ni ikiwa utajiandikisha tarehe 29, 30 ya 31 ya mwezi, na unatozwa bili katika mwezi ambao hauna tarehe hizi. Katika hali hii, utatozwa mapema.

K.m. Ikiwa ulijiandikisha kwenye Showmax tarehe 31 Januari, utatozwa tarehe 28 Februari, 31 Machi na 30 Aprili.


Je, maoni haya yamekufaa?