Unaweza kuendelea kutozwa hata baada ya kughairi usajili wako wa Showmax kwa sababu mbalimbali.
Umeghairi akaunti, si malipo ya moja kwa moja
Ikiwa ulighairi usajili wako wa Showmax lakini bado unatozwa, huenda hujakamilisha kikamilifu utaratibu wa kughairi. Tunapendekeza ujaribu tena kughairi na uhakikishe kuwa umepokea uthibitisho wa barua pepe mara tu unapomaliza. Unaweza pia kughairi malipo yako ya moja kwa moja na benki yako.
Una zaidi ya akaunti moja ya Showmax
Unaweza kuwa na akaunti zingine zinazotumika za Showmax. Kwa mfano, unaweza kuwa umejiandikisha kwa Showmax kwa kutumia anwani mbadala ya barua pepe au nambari ya simu ya mkononi. Tunapendekeza uangalie anwani zingine zozote za barua pepe na uhakikishe kuwa umeghairi usajili wote.
Mtu mwingine alianzisha upya usajili wako
Kuna uwezekano kwamba mtu fulani ameanzisha upya usajili wako wa Showmax kimakosa. Tunapendekeza uondoke kwenye vifaa vyako vyote na uweke upya nenosiri lako ili uhakikishe kuwa hakuna mtu mwingine anayeweza kuanza kutumia akaunti yako ya Showmax, kabla ya kujaribu tena kughairi.
Ikiwa unahitaji usaidizi zaidi kuhusu kughairi kwako au malipo yasiyotarajiwa, tafadhali Wasiliana Nasi.