Fuata hatua hizi ikiwa ulipoteza uwezo wako wa kuingia katika akaunti yako ya Showmax:
- Nenda kwenye showmax.com/forgot.
- Andika anwani ya barua pepe ambayo imeunganishwa na akaunti yako ya Showmax. Chagua Endelea.
- Angalia barua pepe zako upokee maelekezo kuhusu jinsi ya kubadilisha nenosiri lako.
- Fuata maelekezo yaliyo katika barua pepe ili kubadilisha nenosiri lako na kulihifadhi.
Tafadhali kumbuka kuwa kiungo kitatumika kwa saa 3 tu baada ya kutuma ombi.
Usipopokea kiungo cha kubadilisha nenosiri, angalia sehemu ya barua taka au ubofye kitufe cha Tuma tena.
Vidokezo vya kuweka nenosiri thabiti
Hivi hapa vidokezo vya kuweka nenosiri thabiti:
- Weka nenosiri la urefu wa angalau herufi 10.
- Tumia mchanganyiko wa herufi, nambari, herufi kubwa na herufi maalum.
- Usiweke taarifa za kibinafsi na majina halisi.
- Kumbuka, nenosiri lisilo rahisi litakuwa thabiti zaidi.
Ikiwa unahitaji usaidizi zaidi wa kuingia, tafadhali wasiliana nasi.