Kituo cha Usaidizi

Nitapataje Akaunti ya Showmax iliyopotea?


Ni kawaida kusahau maelezo yako ya kuingia kwenye akaunti. Usijali, tuna vidokezo vichache vya kukusaidia kurejesha akaunti yako ya Showmax:

 

Angalia anwani mbadala za barua pepe na namba za simu

Ikiwa una barua pepe zaidi ya moja au namba ya simu, angalia ikiwa umejisajili kwenye Showmax ukitumia hizo. 

 

Angalia ikiwa kuna makosa ya tahajia

Makosa ya tahajia hutokea! Hakikisha umeweka anwani yako ya barua pepe au nambari ya simu ya mkononi, na nenosiri kwa usahihi.

Iwapo bado huwezi kuingia, jaribu kuweka upya nenosiri lako au ujaribu kuingia ukitumia namba yako ya simu ya mkononi badala ya anwani ya barua pepe yako.

Iwapo unashuku kuwa kulikuwa na makosa ya kuandika barua pepe au nambari yako ya simu ulipojiandikisha, tafadhali Wasiliana Nasi ili tukusaidie zaidi.  


    Je, maoni haya yamekufaa?