Kituo cha Usaidizi

Tatua matatizo wakati unapojisajili kwenye Showmax


Je, una matatizo unapojisajili kwenye Showmax? Angalia matatizo ya kawaida hapa chini ili upate hatua za utatuzi  

Ninaona ujumbe ukisema kwamba tayari nimefungua akaunti kwa kutumia anwani yangu ya barua pepe au simu ya mkononi

Kila akaunti ya Showmax lazima iwe na anwani ya kipekee ya barua pepe na nenosiri linalohusishwa nayo. Ikiwa unahitaji kufungua akaunti mpya, jaribu kutumia anwani tofauti ya barua pepe au nambari ya simu ya mkononi.

Tayari nina akaunti ya Showmax

Ikiwa tayari una akaunti, ingia tu kwa kutumia vitambulishi vyako! 

Ikiwa una matatizo wakati wa kuingia, angalia Matatizo ya Kuingia kwenye akaunti ili upate hatua za utatuzi, au kama hukumbuki vitambulishi vyako, angaliaNitapataje Akaunti ya Showmax iliyopotea?

Ukishaingia katika akaunti, unaweza kuanzisha upya usajili wako,kubadilisha mipango, kubadilisha njia yako ya kulipa au kuanza kufurahia maudhui yako!

Nimeanza kujiandikisha lakini sikukamilisha hatua zote

Ikiwa ulianza kujiandikisha na tayari umefungua akaunti yako, sio lazima uanze tena tangu mwanzo. Ili kukamilisha kuweka mipangilio:

  1. Nenda kwenye Showmax.com kisha uingie kwenye akaunti.
  2. Nenda kwenye Akaunti kupitia upau wa menyu wa juu kulia.
  3. Chagua Mipango na Malipo.
  4. Katika sehemu ya Ongeza Mpango, bofya kitufe cha Ongeza Mpango.
  5. Chagua mpango wako na ufuate maagizo ya kulipa.

Ninapata matatizo ya kulipa

Tazama Nitafanyaje ikiwa njia yangu ya kulipa imekataliwa? ili upate hatua za kutatua, au angalia Ninawezaje kulipia Showmax? ili upate njia mbadala za kulipa.


Je, maoni haya yamekufaa?