Kituo cha Usaidizi

Je, Intaneti yangu inahitaji kuwa na kasi kiasi gani ili utumie Showmax?


Ili unufaike zaidi na utiririshaji wa Showmax, tunapendekeza kasi ya 5.5 Mbps au zaidi. 

 

Jaribu kasi yako ya intanetiili uhakikishe kuwa inakidhi kiwango cha chini kinachopendekezwa. 

 

Hivi hapa vidokezo vichache ambavyo vinaweza kusaidia kuboresha kasi yako ya mtandao: 

 

Karibia kisambaza data chako 

Jaribu kukaribia kisambaza data chako ili uboreshe mtandao. Ikiwa unakumbana na matatizo ya utendakazi unapounganisha kwenye mtandao, kwa ujumla utahitaji kuwa karibu na kisambaza data. Katika maeneo ambapo unakumbana na kasi ndogo au matatizo ya muunganisho, kuongeza kiimarisha intaneti kunaweza kufaa. Fikiria kutumia kiimarisha ishara au kiimarisha mtandao ili uboreshe huduma ya mtandao wako wa Wi-Fi katika nyumba yako yote. 

 

Badili utumie nafasi yenye nguvu zaidi ya chaneli ya Wi-Fi 

Kuchagua chaneli inayofaa ya Wi-Fi kunaweza kuboresha kwa kiasi kikubwa utumiaji na utendakazi wako wa Wi-Fi. Kwa mfano, fikiria kubadili Wi-Fi ya 5GHz, ikiwa inapatikana, ambayo hutoa masafa yaliyopanuliwa. 

 

Badilisha mtandao kutoka kwa Wi-Fi utumie data ya simu 

Unaweza kujaribu kuunganisha kwenye mtandao wako wa data ya simu badala yake. Fikiria matumizi ya data unapotumia data ya mtandao wa simu. Rejelea miongozo rasmi ya kudhibiti miunganisho ya simu za mkononi: 

Tazama au ubadilishe mipangilio ya data ya simu za mkononi kwenye kifaa chako cha iOS

Punguza na udhibiti matumizi ya data ya simu za mkononi kwenye kifaa chako cha Android
 

Zima na uwashe kisambaza data chako 

Kuzima na kuwasha kisambaza data chako kunaweza kutatua hitilafu za muda, kufuta kumbukumbu, kukamilisha masasisho yoyote ya programu dhibiti, na kuonyesha upya muunganisho wako. Ili uzime na kuwasha kisambaza data chako mwenyewe, kichomoe kutoka kwa chanzo cha nishati, subiri kwa sekunde 30, kisha ukichomeke tena. 

 

Ondoa muunganisho wa vifaa vingine 

Ikiwa vifaa vingine vimeunganishwa kwenye mtandao wako - haswa ikiwa vinatumia kipimo data kikubwa - kuviondoa kunaweza kuboresha kasi yako ya upakuaji. Kasi ya upakuaji inaweza kupungua kwa kuwa vifaa vingi vinatumia pamoja muunganisho wa intaneti. Pia, jaribu kufunga programu zisizo za lazima na uone ikiwa hiyo inasaidia. 

 


Je, maoni haya yamekufaa?